Takriban watu 430 wamekufa
kutokana na wimbi la joto linalovuma nchini India.
Watafiti wamesajili
kiwango cha juu mno cha nyuzijoto 48'C katika maeneo mengi nchini humo.
Vifo vingi zaidi
vimeripotiwa katika majimbo ya kusini ya Telangana na Andhra
Pradesh, ambapo
watu 140 wamepoteza maisha yao kuanzia jumamosi wimbi hilo la joto lilipotokea.
Mji wa Allahabad ulioko
Uttar Pradesh ulisajili vipimo vya nyuzijoto 48C huku wakaazi wa mji mkuu wa
India New Delhi ukistahimili kiwango cha nyuzijoto 44C
Maafisa wa utawala nchini
humo wameanza kampeini ya kuwahamasisha wanainchi kukaa majumbani mwao na
kuwashauri wanye waji mengi.
Yamkini viwango vya joto
vimekuwa juu zaidi katika kipindi cha mwezi mmoja uliopita lakini vifo vimeanza
kuripotiwa mwishoni mwa juma.
Jimbo la Andhra Pradesh
ndilo lililopoteza watu wengi zaidi ikiwa na jumla ya watu 246 waliopoteza
maisha yao kuanzia juma lililopita.
"asilimia kubwa ya
wale waliopoteza maisha ni watu wenye umri wa zaidi ya miaka 50 walioshinda nje
ya majumba yao.'' alisema kamishna wa kupambana na majanga katika jimbo la
Andhra Pradesh.
Wakfu wa waandishi wa
habari wanasema kuwa watu 186 wameaga katika wilaya 10 za jimbo la Telangana.
Watu 58 wamekufa kuanzia
siku ya jumamosi.
Idara ya utabiri wa hali
ya hewa imesema kuwa kuna uwezekano mkubwa kwa hali hiyo ya joto kuendelea kwa
siku kadha zijazo.
Watu wengine kumi
walpoteza maisha yao katika jimbo la Magharibi mwa Bengal.
Waendesha teksi ambazo
hazina kiyoyozi hawataruhusiwa kuhudumu kwa saa
tano katika mji mkuu wa
Kolkata. Hii inafuatia vifo vya madereva wawili.
Idara ya utabiri wa hali
ya hewa inasema kuwa hali hiyo ya juu ya joto inatokana na ukosefu wa mvua.
Credit:BBC SWAHILI