Staa wa sinema za
Kibongo, Kajala Masanja ‘K’ amepatwa na dhahama ya aina yake baada ya kuibiwa
nguo yake ya ndani kimazingara kisha kuikuta nje ikiwa imeloa damu, Ijumaa lina
mchapo kamili.
Kwa mujibu wa chanzo
makini, mara nyingi Kajala ana kawaida ya kufua na kuzianika nguo hizo ndani
lakini katika mazingira ya kutatanisha moja ilipotea na kila alipofanya
jitihada za kuitafuta, hakuiona.
Chanzo
hicho kilizidi kumwaga ubuyu kuwa, baada ya nguo hiyo kutooneka ghafla, Kajala
alichanganyikiwa sababu nyumbani kwake hakuna hata panya ambaye anaweza kuibeba
pengine na kuitupa sehemu nyingine.
Chanzo hicho ambacho kipo karibu sana na Kajala kilizidi kutiririka kuwa, baada
ya kulitafuta ‘kufuri’ hilo kwa muda mrefu bila mafanikio, alikuja kulikuta
kwenye ndoo tupu ya maji tena ikiwa imetobolewa huku ikiwa imetapakaa damu.
“Baada ya Kajala kuona hivyo alipandwa na presha kwa kuwa hakutegemea
kuiona ikiwa katika hali kama hiyo,” kilidai chanzo hicho.Baada ya chanzo hicho
kuweka nukta, Ijumaa lilimvutia waya Kajala ili kuweza kupata undani zaidi wa
tukio hilo:
Ijumaa: Pole Kajala na mkasa uliokupata.
Kajala: Mkasa gani tena jamani.Ijumaa: Si wa kuibiwa nguo yako ya ndani na kuikuta imetobolewa huku ikiwa na damu!Kajala(Mshangao) hiyo habari mmeipata wapi nyie kweli dunia haina siri, yeah! Ni kweli ilitokea lakini sitaki kuizungumzia sana hivi vitu si vya kuanika kila mtu ajue, nashukuru Mungu kwa kunipigania.
Chanzo: GPL