SIYO siri! Huku jana akiwa ametarajiwa kuripoti tena Kituo
Kikuu cha Polisi, Dar (Central) kauli ya serikali kwamba, taasisi za dini
ambazo viongozi wake wamekuwa wakitoa matamshi yenye mlengo wa kisiasa zitafutwa
mara moja kwani ni kinyume na sheria ya usajili inadaiwa kumpa presha Mchungaji
wa Kanisa la Ufufuo na Uzima, Josephat Gwajima.
Juzi,
gazeti hili lilizungumza na baadhi ya waumini wa makanisa mbalimbali ya kiroho
ya jijini Dar ambao walieleza kuwa, kauli hiyo inamgusa Mchungaji Gwajima kwa
vile ndiye ambaye hivi karibuni alitoa maneno yenye mweleko wa kisiasa.
“Mimi nadhani Gwajima ndiye mwenye presha. Maana yote
yaliyosemwa ndiyo ambayo yeye amehusika nayo, kuhusu maneno ya kisiasa na
mrejesho wa uendeshaji wa kanisa lake, mambo ambayo ametakiwa kuwasilisha
baadhi ya nyaraka pale Alhamisi ijayo (jana) kwenye Kituo cha Polisi cha
Central,” alisema Yohana Petro, mkazi wa Mwenge.
Akizungumza na gazeti hili kwa sharti la kutotajwa jina lake,
mchungaji mmoja wa kanisa la Gwajima alidai:
“Watu wanaweza kufikiria kwamba Mchungaji Gwajima ana presha lakini sidhani kama hali iko hivyo. Suala la viongozi wa dini kutoa matamko ya kisiasa ni la kidunia. Viongozi wa dini wanatakiwa kukemea maovu ya nchi.
“Watu wanaweza kufikiria kwamba Mchungaji Gwajima ana presha lakini sidhani kama hali iko hivyo. Suala la viongozi wa dini kutoa matamko ya kisiasa ni la kidunia. Viongozi wa dini wanatakiwa kukemea maovu ya nchi.
“Gwajima yuko imara, yupo ngangari na Neno la Mungu. Yeye ni
mwakilishi wa kazi za Mungu kwa wanadamu!” alisema mchungaji huyo.Jumanne
iliyopita, Waziri wa Mambo ya Ndani, Mathias Chikawe akizungumza na waandishi
wa habari jijini Dar, alisema kuwa, sheria ya usajili wa taasisi za dini
zinakataza viongozi wake kujihusisha na mambo ya kiimani.
credit:GPL