Sehemu ya mabaki ya Helikopta
baada ya kuanguka Ajali ya Helicopter ambayo imedaiwa kuwa ni mali ya Maliasili
na Utalii imegharimu maisha ya marubani 3 wa Jeshi la Polisi Tanzania. Sp Kidai
Kaluse, Insp.Simba Must Simba, Pc. Josso Selestine, Na rubani mmoja Capt.
Khalfan,Ajali hiyo imetokea huko Kipunguni B Moshi Bar,Ukonga-Ilala jijini Dar
es Salaam. Chanzo cha ajali hiyo bado hakijajulikana mpaka sasa.
Kamanda wa
Polisi Kanda Maalumu ya Dar es Salaam, Suleiman Kova akifafanua
jambo mbele ya Vyombo vya habari katika eneo la ajali,kufuatia kutokea kwa
ajali hiyo iliyopelekea vifo vya watu wanne.
Baadhi ya Wataalamu wakifanya uchunguzi wa chanzo cha ajali hiyo ya Helikopta.
Baadhi ya watu wakishuhudia mabaki ya helikopta hiyo iliyopata ajali maeneo ya Kipunguni B Moshi Bar,Ilala jijini Dar es Salaam