UFUATAO ni
ujumbe mfupi wa Muadhama Polycarp Kardinali Pengo alioutoa leo katika Kanisa la
St. Joseph jijini Dar es Salaam kuhusiana na waraka wa maaskofu uliotolewa hivi
karibuni kwa Wakristo nchini kujiandikisha kikamilifu na kisha kuikataa Katiba
Inayopendekezwa wakati wa kura ya maoni kwa vile haikujadiliwa kiuadilifu.
"Maaskofu
hatuna mamlaka ya kuwaamulia/kuwalazimisha waumini wetu wafanye uamuzi gani
kuhusu katiba, kuwaamulia ni kuwadharau kuwa hawawezi kufanya uamuzi sahihi wao
wenyewe na kuingilia uhuru wao.
Waraka huu
unaleta utengano katika taifa kuwa Wakristo, tumechukua uamuzi dhidi ya
serikali na wengine....
Tuwaache
waumini wafanye uamuzi kwa tafakari yao binafsi bila shinikizo letu.....
Wakati
hili linajadiliwa nilikuwa Italy katika kusimikwa makardinali na baadaye India,
wengine wakavumisha nimelazwa,..wengine nimefariki, lakini namshukuru Mungu
hizo ni dua za kuniongezea maisha marefu na afya (makofi).
Nililetewa
waraka nikausoma, umepitishwa baada ya tafakari kubwa nauheshimu. Lakini
nadhani tuwaache waumini wafanye uamuzi kwa uhuru baada ya kutafakari....
Si sahihi
tukaenda katika katiba kama Wakristo kwa shinikizo la kupinga katiba...
Wawe huru
anayepinga kwa hiari yake anayekubali kwa dhamiri yake....
Sidhani
kama viongozi wa dini sasa tuna amri ya kulazimisha uamuzi juu ya katiba....