Wakazi wa
Kigoma Kaskazini leo walikusanyika pamoja kumsikiliza Mbunge wao Zitto
Kabwe ambaye siku ya leo ameamua kuitumia rasmi kama kuwaaga wananchi
na wapiga kura wa jimbo lake.
Zitto
Kabwe ambaye Ijumaa ya wiki hii kupitia mtandao wa kijamii kwenye
akaunti yake ya Twitter ali break news kwamba hatogombea tena Ubunge
kwenye uchaguzi ujao wa mwishoni mwa mwaka huu.
Baada ya
hotuba yake kumalizika,Mtandao huu ulifanikiwa kuongea na baadhi ya
wananchi lakini asilimia kubwa ya wananchi hawajamuunga mkono kwa uamuzi
huo wa Mbunge wao Zitto Kabwe wa kutogombea tena ubunge na wengine
walikwenda mbali zaidi na kusema kuwa kazi bado haijaisha, pia katika
hotuba yake hiyo alisema kuwa ndani ya wiki inayoanza kesho watu
watarajie makubwa na wala wasishtuke kutokana na uamuzi atao uchukua.
Kwa
tetesi zilizo chini ya kapeti hapa mjini Zitto Kabwe anataka kuja
kugombea jimbo la kigoma mjini, hizi ni baadhi ya picha mtu wangu.
Bonyeza {HAPA} kusoma Hotuba yake aliyoitoa leo jimboni kwake kwa kirefu zaidi