MKONGWE kwenye soko
la ugizaji Bongo, Salome Urassa ‘Thea’ amefunguka kuwa miaka ya hivi karibuni
wasanii hawaishi pamoja kama zamani kwani shetani amewaingilia katikati na
kuwatenganisha
Akizungumza na
mwanahabari wetu, Thea alisema kipindi cha nyuma wasanii walikuwa waipenda sana
kuwa na kundi moja wakakaa pamoja na kuelewana lakini kukatokea kitu ambacho
mpaka leo hakieleweki wakasambaratika.“Naamini kuna vitu tulikosea, tunateseka
kweli. Tunatakiwa kabisa kumrudia Muumba wetu kwa kuwa hakuna cha Bongo Movies
wala nini na ninaona inaelekea kufa kabisa lazima tukae na kujikagua upya,”
alisema Thea.
Credit:GPL