Nyota wa muziki Rehema Chalamila, Ray C.
WAKATI staa wa Bongo
Movie, Wema Sepetu akiweka wazi kuwa hawezi kupata ujauzito huku Judith Wambura
‘Jide’ naye akisumbuliwa na tatizo hilo, nyota wa muziki Rehema Chalamila, Ray
C amefunguka na kusema kuwa hali ya kukosa mtoto ambayo ni sawa na ugumba,
inamtesa, kwani katika umri wake wa miaka 33, hajabahatika kuwa naye,Risasi
Jumamosi linakujuza.
Akizungumza
na gazeti hili juzikati, Ray C alisema kuwa pamoja na hamu yake ya muda mrefu
ya kupata mtoto, lakini ameshindwa ingawa anaamini siku yoyote Mungu
atamuwezesha jambo hilo.“Hao kina Jide, Wema mi naona kama ni cha mtoto. Katika
uhusiano wangu wa kimapenzi tangu nivunje ungo, nimewahi kushika mimba mara
moja tu, wakati huo nikiwa na Mwisho Mwampamba, lakini bahati mbaya ilitoka,
tokea hapo sijapata tena,” alisema staa huyo ambaye yupo katika mapambano ya
kuacha matumizi ya madawa ya kulevya.
Alisema katika umri wake huo anatamani sana kuwa na mtoto, kwani
wasichana aliozaliwa nao wakati mmoja hivi sasa wanao watoto wawili hadi
watatu, kitu ambacho kinamuumiza.Alipoulizwa kama matumizi ya dozi ya kuacha
madawa ya kulevya inachangia tatizo lake hilo, alisema siyo kweli, kwani
miongoni mwa ‘mateja’ wenzake anaokunywa nao dawa, wapo wajawazito na wengine
wenye watoto.
Hata hivyo, alisema umri wake siyo mkubwa sana kukata tamaa ya
kutozaa kwani wapo baadhi ya watu hupata ujauzito na kuzaa katika umri wa miaka
45 na kuendelea.“Sidhani kama umri ni sababu, nafikiri bado nina muda wa kuzaa
na kumlea mwanangu nikijaaliwa kuwa naye, lakini pia huwa siishi kumshukuru
Mungu kwa hivi nilivyo maana yawezekana kuna jambo ananiepusha nalo,” alisema.
“Kitu kingine kinachonifanya nisipate mtoto mapema ni pamoja na
kutopata mwanaume aliyetulia ambaye ninaweza kuzaa naye, nadhani nikimpata
mambo yanaweza kwenda vizuri.”Ray C anaingia katika orodha ya masupastaa ambao
licha ya umri wao kuwa mkubwa, lakini bado hawajabahatika kupata watoto, baadhi
yao wakiwa ni pamoja na Judith Wambura ‘Lady Jaydee’, Baby Madaha na Jacqueline
Wolper.
Credit:GPL