Watu nane wamekufa na
mamia kukosa makazi kutokana na mvua kubwa zinazonyesha katika jiji la Dar es
Salaam nchini Tanzania.
Kwa mujibu wa Mwandishi wa
BBC Aboubakar Famau aliyepo jijini Dar es Salaam mvua hizo zimekuwa zikinyesha
mfulullizo na kusababisha uharibifu mkubwa wa miundo mbinu pamoja baadhi ya
watu kukosa makazi yao.
Kumekuwa na foleni kubwa
ya magari na baadhi ya watu wamechelewa kwenda na kurudi kazini.
Mamlaka ya hali hewa
nchini imetahadharisha kuwa mvua hizo zinaweza kuendelea japo zitapungua
kidogo.