Staa anayevuna fedha
nyingi kupitia kipaji chake cha muziki, Bongo, Nasibu Abdul ‘Diamond’.
Staa anayevuna fedha nyingi kupitia kipaji chake cha muziki, Bongo, Nasibu
Abdul ‘Diamond’ amewatelekeza watoto katika Shule ya East Africa International
jijini Dar ambao aliahidi kuwalipia ada, Risasi Mchanganyiko linakuwa la kwanza
kukudondoshea. Chanzo makini kililiambia gazeti hili juzi kwamba, baada ya
Diamond kuwashindanisha watoto hao, Hillary na Hamis (katika picha no. 1 na 2
zilizoko ukurasa wa mbele walipelekwa shule na Diamond) katika shindano la
Ngololo lililonyika Januari, mwaka jana katika Viwanja vya Leaders Club, Dar na
kushinda aliamua kuwapeleka katika shule hiyo na kuahidi kuwalipia ada kila
mwaka lakini kuanzia hapo aliwatelekeza.
“Jamani Diamond kila kukicha anafanya shoo za mamilioni lakini
Wanafunzi wanaodaiwa
kutelekezwa na Staa anayevuna fedha nyingi kupitia kipaji chake cha muziki,
Bongo, Nasibu Abdul ‘Diamond’.ameshindwa kuwalipia ada wale watoto ambao
aliahidi kuwasomesha. Wamesoma mwaka mmoja tu, mwezi uliopita walitimuliwa na
sasa wako nyumbani. Inauma sana kwani hawa watoto walitolewa kwenye shule za
kawaida na yeye ndiyo akawapeleka kule,” kilisema chanzo hicho.
WAZAZI WANASEMAJE?
Akizungumza na gazeti hili, mmoja wa wazazi wa wanafunzi hao, Fadhili alisema
watoto wao walitimuliwa shuleni tangu April mwaka huu kwa kuwa, Diamond
hakuwahi kuwalipia ada tangu alipowaingiza pale.“Inauma sana, kwani tangu
watoto wetu watimuliwe tumekuwa tukifuatilia kwa mtu tuliyeambiwa ni msimamizi
wa Diamond (jina lake linahifadhiwa kwa sasa) lakini hatupi jibu la kueleweka.
Nasibu Abdul ‘Diamond
akiwa na wanafunzi hao pamoja na mwalimu wao.
“Tulipewa namba za simu za mameneja wa Diamond, Hamis Taletale ‘Babu Tale’ na Said Fella lakini kila tukiwapigia simu tunaambiwa msanii huyo hayupo Dar, mara amesafiri, mara yuko kwenye shoo, yaani kila siku tunazunguka tu hatujui tufanye nini.
“Tulipewa namba za simu za mameneja wa Diamond, Hamis Taletale ‘Babu Tale’ na Said Fella lakini kila tukiwapigia simu tunaambiwa msanii huyo hayupo Dar, mara amesafiri, mara yuko kwenye shoo, yaani kila siku tunazunguka tu hatujui tufanye nini.
“Tunaomba sana jamani, mtusaidie na nyie waandishi maana watoto wanapitwa na
masomo na isitoshe kabla ya hapo walikuwa wakisoma kwenye shule za kawaida,”
alisema mzazi huyo.
MSIKIE MWALIMU MKUU
Paparazi wetu alifunga safari mpaka shuleni hapo maeneo ya Mikocheni, Dar na
kufanikiwa kuzungumza na Mwalimu Mkuu, Mercy Githirua ambapo alithibitisha
watoto hao kusimamishwa masomo kutokana na kukosa ada.“Tulivumilia kwa muda
mrefu sana kwani tulimwamini Diamond tukawapokea watoto hao na kuanza masomo.
Siku aliyokuja kuwakabidhi hapa shuleni aliomba ‘invoice’ kwa ajili ya
kututumia ada lakini yuko kimya mpaka leo.
“Hata fedha ya kuwashonea sare za shule ilibidi niwasiliane na (linatajwa jina,
linasitiriwa) maana tunafanya naye kazi nyingi, akatoa hizo fedha lakini ada
ndiyo ikawa tatizo. Hivyo ilipofika Aprili 14, mwaka huu ilibidi niwarudishe
nyumbani mpaka kieleweke kwa kweli.
“Sijapenda tabia ya Diamond, hivi anajua watoto wakimchukia itakuwa ni hatari
sana kwake? Watoto wa watu walikuwa wanasoma huko akaenda kuwatoa na kuwaleta
hapa lakini amewatelekeza, siyo vizuri kabisa,” alisema mwalimu mkuu huyo.
WANADAIWA SHILINGI NGAPI?
Kwa mujibu wa mwalimu mkuu huyo, watoto hao tangu walivyoingia Januari 21, 2014
hawakuwahi kulipiwa ada yoyote hivyo kila mmoja anadaiwa shilingi milioni moja
na laki sita (1,600,000)
DIAMOND, MAMENEJA WAKE!
Juzi, gazeti hili lilifanya jitihada za kumtafuta Diamond kwa njia ya simu
lakini ilikuwa imesetiwa kwamba inafanya kazi muda wote ‘bize’ hata alipotumiwa
meseji hakujibu. Vivyo hivyo kwa mameneja wake, Fella na Bab Tale simu zao
ziliita bila kupokelewa.
TUJIKUMBUSHE
Mwaka jana, Diamond aliandaa shindano la Nani Anaweza Kucheza Staili ya Wimbo
wa Ngololo ambapo watoto kibao walijitokeza Leaders Club. Watoto hao wawili
waliibuka kidedea kwa kuonesha uwezo mkubwa wa kucheza na ndipo zawadi yao
aliamua kuwapeleka kwenye shule hiyo na kukutwa na yaliyowakuta!