VIDEO Queen, mwenye umbo
la aina yake, Agness Gerald ‘Masogange’ amefunguka kwa kinywa chake kuwa
wabunge wawili wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania wanamnyima usingizi kwa kuwa
wanamsumbua kila kukicha wakimtaka kimapenzi.
Video Queen, mwenye umbo la aina
yake, Agness Gerald ‘Masogange’. Akizungumza na mwandishi wa habari hii
Masogange alisema usumbufu wa viongozi hao unamkosesha amani.
“Sijawahi kuona wabunge ving’ang’anizi kama hao, mpaka kuna kipindi nafikiria labda wanaambiana maana anaweza mmoja akakusumbua mchana kutwa, mwingine usiku unashindwa kulala ni simu tu,” alisema Masogange.
Alishangaa wakati wakimsumbua usiku ni wapi wake zao wanakuwa wapi, kiasi cha
kutia shaka kuwa huenda hiyo ndiyo sababu mambo mengine kwenye nchi hayaendi
sawa kabisa.