Wednesday, 18 March 2015

WEMA AZUA TIMBWILI KISA ALI KIBA




Na Musa Mateja/Risasi Mchanganyiko
BOSS Lady wa Kampuni ya Endless Fame, Wema Isaac Sepetu ‘Madam’ amesababisha timbwili la aina yake hivi karibuni, akidaiwa kuwa kwenye harakati za kutaka kukaa karibu na staa wa Bongo Fleva anayesumbua na wimbo wa Chekecha Cheketua, Ali Saleh ‘Kiba’, Risasi Mchanganyiko limesheheni mchapo kamili.

 Boss Lady wa Kampuni ya Endless Fame, Wema Isaac Sepetu ‘Madam’.

NI ARUSHA
Tukio hilo la aina yake lilitokea hivi karibuni kwenye Ukumbi wa Triple A, jijini Arusha ambapo mrembo huyo wa Tanzania mwaka 2006 alienda kwenye sherehe ya mmoja wa rafiki zake huku yeye akipewa ‘taito’ ya mgeni rasmi.


TUJIUNGE NA CHANZO
Chanzo makini kilidokeza kuwa hivi karibuni, Kiba alikuwa na shoo maalum mjini Arusha ambayo ilihudhuriwa na mamia ya wakazi wa jiji hilo ambapo siku hiyohiyo, Wema naye alikuwa  na marafiki zake wakisherehekea na wenyeji wake, hivyo baada ya kuisha na  kusikia Kiba yupo mjini hapo, akaona ni fursa nzuri ya kwenda kumuona.
“Wema alialikwa na rafiki yake  mmoja hivi huku Arusha sasa baada ya sherehe yao kuisha na kuambiwa Kiba anaangusha shoo, akaona bora aibuke Triple A akamuone,” kilisema chanzo hicho.


NI KUMKOMOA DIAMOND?
Katika aya nyingine, chanzo hicho kilimwaga ubuyu kuwa, Wema aliamua kwenda kwenye shoo hiyo ya Kiba akiamini atamrusha roho zilipendwa wake, Nasibu Abdul ‘Diamond’ ambaye anadaiwa kuwa haziivi na Kiba.
“Nasikia Wema alitaka kwenda ukumbini ili ikiwezekana apige mapicha ya kumwaga na Ali Kiba ili yakivuja yamuumize Diamond,” kilisema chanzo hicho.


Staa wa Bongo Fleva, Nasibu Abdul ‘Diamond’.

TEAM KIBA WAMZUIA
Chanzo hicho kilizidi kutiririka kuwa, baadhi ya wapambe wa Kiba (Team Kiba) waliposhtukia mchezo huo, walimzuia Wema getini ili asiweze kuonana naye.

“Wema alikuja majira ya saa 7:45 usiku akiwa na timu yake, kufika pale walitaka kuingia, lakini kwa hali aliyokuwa nayo wakakataa kumruhusu. “Walijua lazima angefanya kitu kwa Kiba, kitendo ambacho wao hawakupenda, hivyo mabaunsa wakafanya kazi yao vizuri.
“Kitendo cha kumkatalia kuingia kilisababisha kizaazaa hasa kutoka kwa wapambe wake. Ilitokea patashika nguo kuchanika kabla ya kukubali yaishe na kuondoka zao,” kilisema chanzo hicho.

BOFYA HAPA KUMSIKIA WEMA
Baada ya kuvutiwa waya na kusomewa mashtaka, Wema alitiririka; “Ni kweli nilikuwa Arusha kwa shughuli zangu, nilifikia Mount Meru ambayo pia baadaye Kiba naye alifikia na tulionana, usiku kulikuwa na pati ya marafiki zangu, tukawa huko tulipomaliza tukaenda kwenye shoo ya Kiba.

Staa wa Bongo Fleva anayesumbua na wimbo wa Chekecha Cheketua, Ali Saleh ‘Kiba’.

“Kwa kweli sikumbuki chochote maana siku hiyo nilikuwa nimelewa sana, kwa hiyo nashindwa kusema kama unachosema nilikifanya au la, ila kesho yake niliambiwa kuwa tulikwenda kwenye shoo ya Kiba na hatukuingia.

“Hata wakati wa kurudi hotelini kwetu sikujua nilifikaje, zaidi ya kesho yake asubuhi niliwasikia kina Martin wakisema kwamba tulienda Triple A lakini kweli hatukuingia kutokana na fujo zilizokuwa zimejitokeza pale hivyo tukaamua kurudi kulala.”


Chanzo: GPL