Bungeni Dodoma leo, Naibu
Waziri wa Fedha Mwigulu Nchemba, ameiagiza Bodi ya Mikopo ya Elimu ya Juu
kuwalipa Wanafunzi ambao hawajapewa fedha zao za kujikimu hivyo na kusababisha
usumbufu kwa wanafunzi hao.
Nchemba aliyasema hayo
wakati akitoa taarifa ya muongozo iliyoombwa na Mbunge wa kuteuliwa viti
maalumu, Esther Bulayo aliyetaka kujua ni nini kauli ya serikali baada ya
wanafunzi zaidi ya elfu 7 wa chuo kikuu cha Dar es Salaam kugoma kushinikiza
kupewa fedha zao toka bodi ya mikopo.
Naibu waziri Nchimbi
alisimama na kuomba radhi wanafunzi kutokana na usumbufu uliojitokeza, na
kusema tayari wizara yake imeshatoa fedha kwa ajili ya malipo kwa wanafunzi
wote wa vyuo ambao hawajalpatiwa fedha zao.
”Naagiza vyombo
vinavyoshughulikia maswala ya elimu kuwalipa haraka wanafunzi ambao hawajapewa
fedha zao ili kuwaepushia usumbufu vyuoni”, alisema Nchimbi .
Jana wanafunzi wa chuo
kikuu cha Dar es salaam waligoma kuingia darasani kutokana na kukosa hela za
kujikwimu, huku wale wa chuo cha Mtakatifu Joseph nao wakigoma kushinikiza
kurudishwa kwa wanafunzi wenzao wa mwaka wa kwanza kurudishwa chuoni baada ya
kugoma kutokana na kucheweleshwa kupewa fedha zao toka Bodi ya Mikopo.