Baada ya kula
viapo vya kutozikana, wasanii wawili wa filamu Bongo, Wema Isaac Sepetu ‘Madam’
na Aunt Ezekiel Grayson wamejikuta wakiangua vilio wakati wakipatanishwa na
rafiki yao mkubwa ambaye ni pedeshee anayejulikana kwa jina la Daudi Mambya.
Habari kutoka
kwa shuhuda wetu zilieleza kwamba, tukio hilo lilijiri wikiendi iliyopita
kwenye Ufukwe wa Coco jijini Dar ambapo Daudi aliwaita kwa mwaliko wa mishikaki
bila wenyewe kujua kinachoendelea.
Habari
zilieleza kuwa, Daudi ambaye kwake huwa hawafurukuti, amekuwa akiumizwa mno na
tofauti ya wasanii hao kwa sababu ni watu walikuwa wakipendana hivyo kugombana
kwao kulikuwa kunaleta shida kwa marafiki zao wengine.
Imefahamika kwamba, Daudi alitumia ujanja wa kuzungumza na kila mmoja kwa
wakati wake ambapo alibaini kuwa hakuna aliyekuwa tayari kupatana na mwenzake.
Ilisemekana
kuwa, Daudi alitumia ujanja wa kitaalamu ili kila mmoja kumuweka sawa bila
kujijua.
“Unajua Daudi ni rafiki yao sana, sasa hakuwa anapendezwa na tatizo ambalo
limejitokeza hivyo alitumia njia tofauti ili kuweza kuwakutanisha pamoja tena
waweze kupatana,” alieleza mtoa habari huyo.
Ilielezwa
kwamba Daudi alianza kwa kumtafuta Wema na kumpeleka Coco Beach akimuambia kuwa
anataka akamnunulie mishikaki huku wakati huohuo akimwambia Aunt naye wakutane
ufukweni hapo.Shushushu wetu alizidi kufunguka kuwa Daudi alitangulia Coco na
Wema, huku akifanya mawasiliano na Aunt na baada ya muda, Aunt naye aliwasili
huku kila mmoja akibaki katika mshangao usioelezeka baada ya kukutana uso kwa
uso.
Sosi huyo
alisema kuwa Wema na Aunt walipoonana kila mmoja alikuwa kimya lakini Daudi
aliamua kuwasomea risala ndefu iliyomwingia kila mmoja.Mambo yakipokaa vizuri,
wawili hao walishuhudiwa wakiwa wamekumbatiana huku kila mmoja akiangua kilio
kilichochukua takribani nusu saa hivyo kufanya eneo hilo kuwa kama kuna msiba.
“Yaani mpaka
Daudi mwenyewe alidondosha machozi baada ya Wema na Aunt kukumbatiana na kuanza
kulia.
“Yaani ilikuwa simanzi kubwa sana,” alimalizia shuhuda huyo.Akizungumza na
gazeti hili, Daudi alisema kuwa aliamua kuwapatanisha wawili hao kwa kuwa
alikuwa hapendezwi na tatizo hilo na kwamba wote ni rafiki zake.
Kwa upande
wake, Aunt alifunguka ya moyoni:
“Tulipokutana kila mtu alijua tatizo lake na tukaona ni mambo ya kijinga,
ikabidi tuweke tofauti pembeni maisha yaendelee.”
Wema alisema:
“Mambo ya kugombanagombana hayana msingi na kwa vile ni mtu mzima (Daudi)
aliwakutanisha, nikaona yaishe.”Wema na Aunt ambao walikuwa marafiki wakubwa
waliingia kwenye mgogoro hivi karibuni baada ya Wema kumtuhumu Aunt kuunga
mkono shoo ya Zari All White Party ya mwanadada Zari Hassan ‘Zari The Boss
Lady’ ambaye ni mpenzi wa aliyekuwa mpenzi wa Wema, Nasibu Abdul ‘Diamond
Platnumz’.
Chanzo: GPL