Kocha mkuu wa Klabu ya
Manchester United Louis van Gaal amewapiga mkwara mzito wachezaji wake
walioibuka na tuzo za msimu za Klabu hiyo huku pia akitoa tahathari kwa
wachezaji wote wakubaliane na matokeo ya uongozi utakao amua ni mchezaji gani
atabaki na nani ataondoka kwa ajili ya msimu ujao.
Mapema kabla ya utoaji wa
tuzo haujachukua mkondo wake, Van Gaal aliwaonya wachezaji wake kutolewa sifa
walizozipata kupitia mchakato wa kumsaka mshindi wa tuzo za mwaka na badala
yake wanatakia kukaza buti kwa lengo la kufanya vizuri msimu ujao wa ligi.
Amesema ni wakati mzuri
kwao kujiapanga kufanya maandalizi ya kutosha wakati wa kujiandaa na msimu wa
2015-16 na ana hakika endapo kila mmoja atawajibiuka kwa nafasi yake Man Utd
itafikia malengo ya kutwaa ubingwa.
Hata hivyo ametoa
tahadhari ya kufanywa kwa mabadiliko katika sehemu ya kikosi chake, na kuwataka
wachezaji kujitayarisha na jambo hilo ambalo litaamuru baadhi yao kuondoka ili
wengine kusajiliwa.
Tayari meneja huyo kutoka
nchini Uholanzi ameshafikia hatua nzuri ya kukamilisha usajili wa mshambuliaji wa
pembeni wa PSV Eindhoven Memphis Depay.
Tayari mchezaji huyoa meshafanyiwa vipimo vya afya na siku kadhaa zijazo ada
yake ya usajili inayotajwa kufikia paund million 25, italipwa ili taratibu
nyingine za kusainiwa kwa mkataba baina ya pande hizo mbili zichukue nafasi
yake.