Wednesday, 20 May 2015

MR BLUE: UGANDA WAPO TAFOUTI NA SISI KATIKA UTENGENEZAJI WA VIDEO

Msanii Mr blue ambaye wiki mbili zilizopita alikuwa nchini Uganda kwa ajili ya kufanya video na msanii Navio kutoka Uganda alifunguka na kusema kuwa ameona tofauti kubwa sana katika ufanyaji wa video bongo na nchini Uganda.
Amesema kuwa wenzetu kule wanatumia muda mrefu katika kufanya maandalizi hasa ya kufanya setting za vifaa kuliko muda wa kufanya shoooting yenyewe.

Mr Blue alifunguka hayo alipokuwa akipiga stori na kipindi cha Power Jams ya East Africa Radio.

Mr Blue anadai mbali na maandalizi ya muda mrefu yanayofanywa katika kuandaa mazingira mazuri ya kufanya kazi pia amesema kwa upande wake hajawahi kutumia vifaa vyenyewe ubora na ukubwa kama ambavyo ametumia katika kufanya video hiyo ambayo imefanyika nchini Uganda akiwa na msanii wa Uganda Navio.

"Cha kwanza kabisa kitu nilichojifunza kwamba video za wenzetu zinavyofanywa ni tofauti sana na zetu, kule wanaangalia sana kufanya setting wanafanya setting kwa muda mrefu mfano tulifika asubuhi, lakini jamaa walikuwa wakifanya setting zaidi ya masaa matano, na kazi tulifanya kama saa moja hivi lakini hapa kwetu wanashoot mara nyingi sana na kisha wanapata kazi kwenda kuchagua scene ambayo itakuwa nzuri ndiyo wanachagua"

Kutokana na hili wenzetu wanaonesha wapo makini zaidi katika ufanyaji kazi tofauti na sisi, lakini kitu kingine wenzetu wana vifaa ambavyo ni vya kimataifa ambavyo awali sikuwahi kuvitumia vifaa hivyo katika kufanya kwangu muziki.

Mwishoni wa mwaka jana msanii Mr Blue alisema kuwa amegundua mashabiki wanamkubali kutokana na show mbalimbali alizopata mwaka jana na namna ambavyo alikuwa akipokelewa na mashabiki jambo ambalo lilimfanya kutoa kauli kuwa atajitahidi kufanya kazi kwa umakini na ubora ili kuwafurahisha mashabiki wake, na mwanzoni mwa mwaka 2015 Mr Blue alionekana na msanii mkongwe Mr 11 katika studio za Mj Record wakifanya kazi ambapo Mr 11 alikiri wazi kupitia mitandao ya kijamii kuwa Mr Blue alimfanya kurudi studio tena.