Mwanafunzi wa chuo kikuu cha Dar es salaam, Cecilia Mosh
(26) aliyejirusha kutoka ghorofa ya tatu hadi chini kutokana na hofu ya moto
uliotokea katika Hosteli ya Mabibo, amevunjika mfupa wa bega.
Mwanafunzi huyo
alijirusha kupitia dirisha juzi katika harakati za kujiokoa na moto baada ya jengo
la wasichana, Block B kushika moto “Nilisikia kelele za moto nikiwa chumbani na
nilipotpka nje nikakuta moshi umetanda kila kona, baada ya kuona hivyo
nilionona ni vema nijioke kwa kujirusha kutoka ghorofa ya tatu ya bweni hilo
hadi chini kupitia dirishani” amesema Cecilia Mosha.