Mwanamuziki
nguli wa Hip Hop, nchini kutoka Mwanza, Fareed Kubanda ‘Fid Q’ (kulia) akipozi
na Balozi wa Umoja wa Ulaya pamoja na baadhi ya washindi wenzake wakati wa
hafla hiyo.
Fid Q alieleza kuwa, kutunukiwa huko ni baada ya mchango wake kuonekana ikiwemo kutoa elimu kwa watoto wa mitaani na vijana kupitia mashairi.
Tuzo hiyo iliyotolewa Machi 17, alipewa kwa sababu maisha yake yanaendana na uhalisia na watu wengine ikiwemo kusaidia jamii akiwa kama msanii na kutambua mchango wake kwa watu wengine.
Mwanamuziki nguli wa Hip Hop, nchini kutoka
Mwanza, Fareed Kubanda ‘Fid Q’ (katikati) akiwa na Balozi wa Umoja wa Ulaya,
Filiberto Sebregondi (kulia) wakati wa halfa ya kukabidhiwa tuzo hiyo.
Fid Q amekuwa akifanya darasa lililokuwa likijulikana kama UJAMAA
DARASA kwa vijana wa mitaani na wanaofanya vitendo viovu vya matumizi ya
madawa waliweza kujifunza na kuachana na mambo maovu ya awali.
Ambapo amesema pia kwa sasa atarejesha pia darasa hilo kwa vijana kwani
pia muziki wake umekua ukielimisha vijana wengi zaidi na watoto wa
mitaani.
Fid Q ni miongoni mwa wasanii wakubwa waliosaidia muziki wa Hip Hop hapa
Nchini kuendelea kukua zaidi huku watu wa rika zote wakiukubali
muziki wake huo hasa katika mistari yake iliyojaa vina vya maarifa vya
kumsaidia mwanadamu yoyote Yule hapa Duniani, hivyo kwa kutunukia tuzo hiyo
amefuraahia na kushukuru wote wanaendelea kumuunga mkono na kumsapoti.
Alichokiandika Fid Q kwenye ukurasa wake wa Instagram.