Dodoma. Raisi Jakaya Kikwete amesema baadhi ya wakuu wa
wilaya walitemwa kutokana na upungufu, ikiwa ni pamoja na madeni mitaani. Rais
alisema baadhi yao walikuwa wakienda baa wanalewa na ili kuwaondoa ilibidi wake
zao waitwe kuwachunguza.
Raisi Kikwete alisema hayo jana mjini Dodoma alipokuwa
akifungua semina elekezi kwa wakuu wa wilaya 27 wapya walioteuliwa hivi
karibuni. February 18 mwaka huu, Raisi kikwete alifanya mabadiliko ya wakuu wa
wilaya na kutengua uteuzi wa wakuu wa wilaya 12.
Raisi kikwete alisema walikuwepo wenye upungufu na
wengine walikuwa na madeni mitaani huku baadhi yao wakiwa na tatizo la ulevi
kiasi kwamba wakienda baa hulewa kupita kiasi.
Aliwaasa wakuu wa wilaya wapya kuwa wengine ni wadogo ki-umri
lazima wafanane na madaraka waliyopewa.
“Pale ulipo ni role model (mfano wa kuigwa), lazima uwe
na tabia njema kwa kauli, matendo, nidhamu na uadilifu usiotiliwa shaka, “alisema
Raisi kikwete