Monday, 25 May 2015

WAZIRI MKUU WA ZAMANI WA ISRAELI AHUKUMIWA KIFUNGO CHA MIEZI NANE KWA KOSA LA RUSHWA

Waziri Mkuu wa zamani wa ISRAEL, EHUD OLMERT, amehukumiwa kifungo cha miezi NANE jela baada ya kupatikana na hatia ya kupokea rushwa ya fedha kutoka kwa mfanyabiashara mmoja wa MAREKANI, MORRIS TALANSKY. 

Tayari kiongozi huyo anatumikia kifungo kingine cha MIAKA SITA jela tangu mwaka jana kutokana na makosa mengine yanayohusiana na rushwa.

EHUD OLMERT alilazimishwa kujiuzulu mwaka 2009 kutokana na kashfa hiyo ambapo inadaiwa kupokea fedha hizo wakati alipokuwa meya wa mji wa JERUSALEM na mmoja wa mawaziri wan chi hiyo kinyume cha sheria.

Mwanasheria wa OLMERT ameeleza kutoridhishwa na hukumu hiyo na kuelezea nia yake ya kukata rufaa katika mahakama kuu ya nchi hiyo.