Sunday, 24 May 2015

SUALA LA LESENI ZA VILABU VYA VPL 2015/2016 TFF YATOA TAARIFA MPYA

Leo jumapili tarehe 24, Mei 2015 Kamati ya Utendaji ya Shirikisho la Mpira wa Miguu nchini TFF imeketi katika ukumbi uliopo makao makuu ya Shirikisho uwanja wa Karume. Kamati ya Utendaji imepitia masuala mbalimbali na kutoa maamuzi yafuatayo:

CLUB LICENCING (Leseni za vilabu) Kamati ya Utendaji imeiagiza sekretarieti ivisisitize vilabu vya Ligi Kuu umuhimu wa kukamilisha maombi yao ya ushiriki wa ligi kuu kwa msimu wa 2015/16 kwa kuwasilisha fomu za maombi ya Leseni za vilabu TFF. Klabu ambayo haitakamilisha mchakato huo haitaruhusiwa kushiriki ligi kuu ifikapo msimu wa 2015/16.

KOMPYUTA - Kutokana na maamuzi ya mkutano mkuu wa TFF uliofanyika Morogoro ambao uliagiza wanachama wake wapya wapewe kompyuta, agizo hilo limetekelezwa na kompyuta hizo watakabidhiwa wajumbe wa Kamati ya Utendaji wanaotoka kanda hizo ili waziwakilishe maeneo husika. Mikoa hiyo ni Geita, Katavi, Manyara, Njombe na Simiyu.


MFUKO WA FDF - Kufuatia mkutano mkuu wa TFF kuingiza kipengele cha FDF katika katiba yake, kikao cha Kamati ya Utendaji wa mujibu wa katiba kimepitisha kanuni za uendeshaji wa mfuko huo.


Aidha kikao hicho kimeteua wajumbe wafuatao wawe wajumbe wa
tume hiyo
(i)Tido Mhando - Mwenyekiti,
(ii) Deogratius Lyatto - Makamu mwenyekiti
(iii)Ephraim Mafuru - mjumbe,
(iv)Beatrice Singano - mjumbe,
(v)Joseph Kahama - mjumbe
(vi)Ayoub Chamshana - mjumbe.


Pia Henry Tandau ameteuliwa kuwa katibu mtendaji wa mfuko huo