Sevilla kwa mara nyingine
tena wamechukua ubingwa wa EUROPA baada ya kuwatungua Dnipro kwa mabao 3-2 na
kuwa klabu ya kwanza barani Ulaya kwa kushinda taji hilo mara nne kwa matokeo
yanayofanana yaani magoli 3-2 mara hizo zote.
Wahispania hao mara ya kwanza walichukua miaka ya 2006 and 2007 wakati huo
likiitwa Uefa Cup - na sasa wamechukua tena kwa mara ya pili mfululizo huku
Carlos Bacca akipiga mbili na kujihakikishia ushujaa wa mchezo.
Wababe hao wa Unai Emery mwaka jana walishinda kwa mikwaju ya penati baada ya
mchezo kumalizika kwa are ya 0-0 dhidi ya Benfica, lakini wakati huu wamekataa
kabisa kufika huko.
Grzegorz Krychowiak aliipatia Sevilla bao la kwanza huku Bacca akiongeza la
pili na tatu na kuhitimisha ushindi kwa wababe hao wa EUROPA.
Nao Dnipro ambao wanatokea nchini Ukraine walijipatia magoli yao kupitia kwa nahodha wao Ruslan Rotan na Nikola Kalinic.