Mume wa Staa wa filamu za
Kibongo,Irine Uwoya, Hamad Ndikumana ‘Katauti’amesema kuwa hajaachana na msanii
huyo kama ambavyo baadhi ya watu wanavyodhani.
Ndukumana ambaye ni
mwanasoka kwenye klabu moja ya soka nchini Rwanda ameyazungumza hayo hivi
karibuni wakati alipofanya mahojiano na mtangazaji wa Clouds TV, Zamaradi
Mketema alisema kuwa ingawa hawaishi pamoja na Irene Uwoya lakini hawajaachana.
‘Sijaachana na Irene Uwoya ingawa hatuishi pamoja yeye anaishi Dar mie naishi
Rwanda na bado nacheza soka ila nategemea kusomea ukocha baada ya kustaafu
soka,’ alisema Ndikumana.
Irene na Ndikumana walifunga ndoa mwaka 2008 na kubahatika kupata mtoto mmoja aitwaye Krish.