Mrembo mchakarikaji Bongo,
Jokate Mwegelo ‘Kidoti’. Akizungumza na Ijumaa Jokate alisema, watu wanaongea
sana kuhusiana na ukaribu wao bila kujua kuwa Kiba ni mtu wake kitambo na sasa
ndiye kila kitu kwake kwani ana projekti naye kibao ambazo zinakuja na wasioelewa,
ipo siku wataelewa.
MREMBO mchakarikaji Bongo,
Jokate Mwegelo ‘Kidoti’, juzikati aliamua kuvunja ukimya na kusema kuwa
mwanamuziki Ali Kiba kwa sasa ndiye kila kitu katika mambo yake mengi ya
kimaisha
Mwanamuziki Ali Kiba.
“Yaani watu wangu wajue Kiba ni kila kitu kwangu ila siyo ishu ya mapenzi, tuna
projekti kibao, nawaomba watu wavute subi--ra watajionea kila kinachoendelea
kati yetu.Kuanzia sasa Kiba atakuwa akipeperusha ‘brand’ za Kidoti kwa kila atakachofanya
ikiwa ni pamoja na mavazi,” alisema Jokate.