Uongozi wa Simba
umeonyesha umepania kuimarisha safu yake ya ulinzi baada ya kumnasa beki wa
JKT, Mohammed Fakhi, jana usiku.
Faki amesaini mkataba wa miaka miwili kuichezea Simba jijini Dar es Salaam na
Mwenyekiti wa Kamati ya Usajili ya Simba, Zacharia Hans Poppe amethibitisha.
“Kweli Faki amesaini miaka miwili, hii ni sehemu ya kuhakikisha tunaimarisha
safu ya ulinzi,” alisema.
Faki aliichezea JKT kwa ufanisi mkubwa katika msimu uliopita.
Chanzo:Salehjembe
Chanzo:Salehjembe