Thursday 21 May 2015

SAUTI: SERIKALI YATOA TAMKO KUFUNGWA KWA VITUO VYENYE KUONYESHA SINEMA CHAFU (NG***NO)

Leo asubuhi katika kipindi cha mawsali katika wizara mbalimbali za serikali, Mh Betty Machangu  ambaye ni mbunge wa viti maalumu kwa  tiketi ya CCM, aliiuliza serikali ni lini watafafanya operesheni ya kuzuia picha chafu zinozoonyeshwa katika vituo mbalimbali na kuharibu utamaduni na mila za vijana wetu wanaosoma. 

Naibu waziri wa Habari, Utamaduni na Michezo ajibu...
Hili ni jambo ambalo kwa namna moja ama nyengine limeenea sana hasa katika maeneo ya Dar es salaam na baadhi ya miji mikubwa na mimi niombe Mh spika kutumia fursa hii kuziomba halmashauri za wilaya, polisi kuchukua hatua za dhati kabisa dhidi ya vibanda  ambavyo vinaonyesha picha za sinema ambazo ni chafu na mara nyingi wamekuwa wakionyesha baada ya saa nane mchana wakijua fika kuwa wazazi wa wanafunzi wako makazini na ndipo wanafunzi wanapokimbia nyumbani na kwenda kuangalia picha hizi, nirudie tena , kuziomba mamlaka zinazosimamaia maeneo yao kuchukua hatua za haraka ili kuthibiti hali hii.

Bofya kitufe cha kucheza usikie alichokisema Naibu waziri wa Habari, Utamadni na Michezo...