Thursday 21 May 2015

SAUTI:MHE. JOSEPH SELASINI ALIA NA POMBE ‘GONGO’ ATAKA IWE HALALI PIA SERIKALI IOMBE RADHI KWA KAULI YA MKUU WA WILAYA YA ROMBO.


Kama kawaida kwa siku ya Alhamis Bungeni kuna kuwa na masuali ya papo kwa papo kwa Mh waziri mkuu. Leo hii katika masuala ya papo kwa papo, Mh Salasin amemualiza waziri mkuu juu ya biashara ya pombe kuweza kupatiwa kibali halali ili wananchi waendelee kunafaika na biashara hiyo ya pombe “GONGO”.

Mh Salasin afunguka hivi…..

Mh waziri mkuu katika nchi yetu wananchi wetu wana pombe nyingi za kienyeji ambapo kwa namna moja au nyengine zinawasaidia kuongeza kipato katika familia, kusomesha watoto na vile vile kuchangia zaidi katika shughuli za maendeleo.
Mh spika askari wetu hasa jeshi la polisi wamekuwa wakiwabugudhi sana wananchi kwa kuwapiga, kuwakamata na kuwanyanganya vyombo vyao ambavyo wanatumia kwa ajili ya shunguli hii, Ningependa kujua Mh waziri Mkuu kama serikali yetu ina sheria mahsusi au kwa kutumia vyombo vyake kama TBS au TFDA kuweza kuwasaidia wananchi hawa kufanya shughuli hizi zao kitalamu zaidi na kwa sababu, hii ni kama viwanda vidogo vidogo, shunguli hizi ziweza kuongeza ajira kwa watanzania ambao wanazunguka maeneo mbalimbali ambapo pombe hizi zinatengenzwa.

Naye waziri Mkuu alimjibu  Mh Salasin kama ifuatvyo..

Mh spika, Mh salasini amefiicha ficha jambo pale hakulitaka kulisema, ni kweli zipo pombe mbali mbali ambazo watanzannia wanazitumia katik amazingira yetu ya vijijini,eeehh, ukienda Chagani kule tunayo pombe tunaijua vizrui lakin kwa maelezo yake inaonenakana pombe anayoizungumza itakuwa ni Gongo, hasa GOONGO ni pombe ambayo ni kweli kabisa kwa maana ya usimamizi wa utendeji wa serika, serikali imekataza utengenezaji wa hiyo pombe, na kwa hiyo unywaji wa hiyo pombe na msingi wake ni rahisi tu ni kwa sababu viwango vyake ni viwango ambavyo havipimiki kwa kiwango ambacho nasema hiki ndo kiwango wastani ambacho binadamu anaweza akakitumia, ndo mana serikali imekuwa makini, kwa kuhakikisha kwamba pombe hii lazima tuipige vita kwa sababu hiyo, hasa umenipa changamoto, kwamba baada ya kuipiga vita kwanini msitafute utaratibu wa namna wa kuwawezesha watanzania hawa pombe ioi io basi ikatengenezwa kwa viwango vinavyotakiwa halafu muendelee kuitumia kwa maana hiyo,aah! Sasa ilo ni jambo jema lakini mimi si mtaalamu sana wa jambo hili ndo mana sisi tunajua ni kwamba konyagi ni aina ya pombe nyengine vilevile lakini konyagi imepita kwenye mchakato ikathibitika, ikawekewa viwango ndo mana inanyweka kwa namna ambayo tunaamini haina madhara makubwa sana kwa binaadam, kwa io mimi nikubali kuchukua io changamoto sasa sina, labda tuwape watu wa viwanda na biashara labda walitizime waone kama kuna uwezakano gani inawezekana ikawa vile vile ni pengine ni product ambayo unaweza kuipekla kwenye kiwanda chetu cha Konyangi pengine ikafanyiaka, ikafanya kazi ya ziada kidogo kuweza kuiboresha na ikawa kinywaji kizuri siujua lakini kwa sasa ni lazima tuseme watanzania pombe hii ni hatari kwa sababu madhara yake yanajulikana, maeneo mengi yanayotumia pombe hii mara nyingi ndo mauji mengi, mara nyingi kuna matatizo mengi sana ndo mana si vizuri kuiendkeza pombe ya kiwango kile.

Bofya kutufe cha kucheza, usikilize kilichojiri .…