STAA wa filamu za Kibongo,
Salma Jabu 'Nisha' usiku wa kuamkia leo amevamiwa na watu wanaodhaniwa kuwa ni
majambazi wapatao watano nyumbani kwake Kijitonyama jijini Dar na kuporwa
baadhi ya mali.
Kupitia akaunti yake ya
Instagram, Nisha ameandika kuwa majambazi wapatao watano wakiwa na gari
walivamia nyumbani kwake na kumpora huku akimshukuru Mungu maana yeye yuko
salama.
Gari la Nisha likiwa limeibiwa baadhi ya vitu.
Staa huyo pia aliweka
picha ya gari lake lililokuwa limeibiwa baadhi ya vitu na majambazi hao kisha
kuandika hivi:
Tukio hili limetokea ikiwa
ni siku chache baada ya staa wa Bongo Fleva, Ali Saleh Kiba 'Ali Kiba' naye
kuvamiwa na watu wanaodhaniwa kuwa majambazi wapatao 20 nyumbani kwake
Kunduchi, Dar kisha kumpora mali.