Wednesday, 27 May 2015

JOH MAKINI AHIT CHART ZA MTV BASE.

Video ya wimbo ‘Nusu Nusu’ ya Joh Makini imeingia rasmi katika chartza muziki za MTV Base zijulikanazo kama ‘Official African Chart’.
Joh Makini

‘Nusu Nusu’ ni video iliyofanyika nchini Afrika Kusini na iliachiawa rasmi mwezi jana April 26 ambapo mpaka sasa ina mwezi mmoja tangu izinduliwe na kituo hicho cha MTV.

Video ya Nusu Nusu imeingia na kukamata namba 8 kitu ambaco kinaonesha jinsi video hiyo inakubalika.

Aidha Joh Makini anaendelea kufanya vizuri kwa wimbo huo kwani ‘Nusu Nusu’ inafanya vizuri pia katika runinga ya Trace TV ya nchini Ufaransa.