Wednesday, 27 May 2015

UPANDAJI WA NAULI HOLELA YAPATIWA UFUMBUZI, SERIKALI YATOA TAMKO.

Waziri wa uchukuzi Mh Samuel Sita

Waziri wa uchukuzi Mh Samuel Sita, akijibu swali la Mh Kakoso mbunge wa Mpanda vijijini aliyetaka kujua “Je serikali ina mpango gani wa kudhibiti upandeji holela wa nauli kwa usafiri wa mabasi na haisi katika wilaya ya Mpanda”

Waziri wa Uchukuzi afafanua hivi…….

Mh naibu spika jibu la Mhe. Seleiman kakoso mbunge wa mpanda ni kama ifuatavyo.

Mh Naibu spika mamlaka ya uthibiti ,usafiri wa nchi kavu na majini (SUMATRA)  kwa nyakati mbali imekuwa ikililia viwango vya nauli kikomo kwa njia za lami na vumbi.

Viwango vya nauli vinavyotumia kwa sasa viliridhiwa na mamlaka hiyo mnamo mwaka 2013, ambapo kwa mabasi ya kawaida (Ordinary bus) kiwango kilichoidhinishwa ni sh 36.89 kwa kilomita moja ya abiria katika barabara ya lami na sh 46.11 kwa kilomita moja  ya abiria katika barabara ya vumbi, kwa mabasi ya hadhi ya kati (Semi luxury) ni shilingi 53.22 kwa kilomita moja ya abria na mabasi ya hadhi ya juu ni shilingi 58.47 kwa kilomita moja ya abiria.

Mh Naibu spika , nauli za mabasi kwa kuzingatia viwango vilivyoridhiwa hutangazwa na kubandikwa katika maeneo mbalimbali ya wazi ikiwa ni pamoja na maeneo ya vituo vya mabasi, ili kusimamia viwango hivyo ofisi za mikoa za SUMATRA kwa kushrikiana na jeshi la polisi kikosi cha uslama barabarani wamekuwa wakifanya ukaguzi mara kwa mara ili kubaini viwango vinapokiukwa.


SUMATRA  pia imekuwa ikiwataka wananchi kutoa taarifa pale wanapo tozwa nauli inayokiukwa nauli kikomo ili hatua sahihi zichukuliwe zidi ya wahalifu , mamlaka imetoa namba za simu za bure, ili kurahisisha utoaji wa taarifa, namba hizo ni 0800110019 na 0800110020.