Wednesday, 27 May 2015

ACT WAZALENDO KUIBUKA OPERESHENI MAJI MAJI

Kiongozi wa chama cha ACT wazalendo Zitto Kabwe .

Kamati kuu cha ACT waazalendo    imeazimia  kueneza na kujenga chama katika majimbo 59 kwenye mikoa 19, kupiti operesheni I  liyopewa jina la Maji Maji.

Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa  na  Afisa Habari ACT Wazalendo Abdallah Khamis imebainisha kuwa Lengo la operesheni maji maji litakuwa kukagua  uhai wa  chama kazi itakayofanyika kwa siku 12 kwa timu kumi za kazi kujigawa katika maeneo mbali mbali.

Hayo yanafuatia kamati Kuu ya Chama cha ACT-Wazalendo, iliyokuwa na kikao chake cha kawaida cha siku mbili kilichokaa tarehe, 23 na 24 mwezi huu na kilichoongozwa  na Mwenyekiti wa Taifa, Anna Mghwira, pia kilihudhuriwa na kiongozi wa Chama Zitto Zuberi Kabwe ambapo kilikuwa na ajnda za Uteuzi wa nafasi mbali mbali za kiutendaji ndani ya chama, Operesheni majimaji pamoja na Ratiba ya Uchaguzi mkuu na Ngome za Chama.

Katika mkutano kamati kuu  wanachama wafuatao  wameteuliwa:
Manaibu katibu wakuu bara na Zanzibar  ni Msafiri, Abrahaman Mtemelwa na upande wa Zanzibar ni Juma Said Sanani, kuwa Naibu katibu Mkuu Zanzibar
Makatibu wa kamati mbalimbali, Kamati kuu imemteua Peter Mwambuja kuwa katibu wa Fedha na Rasilimali

Nafasi ya wenyeviti, Kamati kuu imemteua Estomih Mallah kuwa mwenyekiti wa Kamati ya Fedha na Rasilimali na Mwanasheria wakili  Albert Msando, ameteuliwa kuwa Mwenyekiti wa kamati ya Katiba na Sheria
Wajumbe Wa Kamati Kuu, Kamati kuu imewateua Mzee Japhari Kasisiko na Hamad Mussa Yusuph


Kwa upande wa washauri wa chama Kamati kuu kwa nafasi yake imewateua Profesa Kitilla Mkumbo na Tery Bermunda(mama Tery) kuwa washauri wa Chama.