Thursday, 21 May 2015

JAMALI MALINZI AMKINGIA KIFUA KOCHA MKUU WA TAIFA STARS (MART NOOIJ), ASEMA HANA MPANGO WA KUMFUKUZA.

Raisi wa shirikisho la mpira wa miguu nchini Jamali Malinzi amesema kuwa hana mpaongo wa kumfukaza kocha mkuu wa timu ya taifa(taifa stars) Mart Nooij, kwa sasa wadau mbalimbali wa soko wamependekeza kufukuzwa kwa kocha huyo hasa kutokana na kufanya vibaya katika michuano ya COSAFA inayoendelea nchini Afrika kusini.

Naye Kocha huyo Mart Nooij amesema..
Nitarekebisha makosa yaliyojitokeza katika michezo kuwania kombe la COSAFA na kupoteza mechi mbili ya kundi B kabla ya kuivaa misri mwezi ujao. 
Tanzania ilipoteza mechi yake ya pili kwa kufungwa na Madagacsa mabao 2-0, katika mchezo wa kwanza taifa stars ilifungwa bao 1-0 na switzerland, matokeo ya mechi kundi B Switzerland  imeitandika lusotho 1-0, Taifa stars ina buruta mkia katika kundi B ikiwa haina alama (point) wala bao na leo inatupa karata yake ya mwisho dhidi ya Lusotho kabla ya kurudi nchini.