Friday, 22 May 2015

SERIKALI YAENDELEA KUTOA TAALUMA YA SHERIA

Naibu Waziri wa Katiba na Sheria UMMY MWALIMU amesema Chuo Cha Uongozi wa Mahakama cha LUSHOTO - IJA, Mkoani TANGA kitaendelea kutumika kutoa taaluma ya sheria huku vyuo vingine vikitoe elimu ya juu ya sheria katika taaluma hiyo. 
Naibu Waziri wa Katiba na Sheria UMMY MWALIMU

Akijibu swali bungeni Naibu Waziri MWALIMU amesema chuo hicho kinatoa mafunzo ya cheti cha sheria na stashahada ya sheria ambapo wahitimu huajiriwa kama makarani na mahakimu na kwamba baadhi ya majaji na mahakimu hupatiwa mafunzo elekezi chuoni hapo. 

Awali Mbunge wa KASULU Mjini, MOSES MACHALI alipendekeza Chuo Cha Uongozi wa Mahakama cha LUSHOTO kisitishe kutoa mafunzo ya mafunzo ya cheti na stashahada ya sheria kwani wahitimu wa mafunzo hayo hukosa ajira kutokana na vyeti hivyo kuwa vya ngazi ya chini