Friday, 22 May 2015

SAUTI: SERIKALI KUTOA BILIONI 866 KUMALIZA UJENZI WA MIUNDOMBINU

Waziri wa Ujenzi Dokta JOHN MAGUFULI amesema Shilingi Bilioni 866 zitatolewa ili kukamilisha ujenzi wa miundombinu ya barabara ikiwa ni sehemu ya utekelezaji wa ahadi za rais alizozitoa katika utekelezaji wa Ilani ya Chama Cha Mapinduzi - CCM. 
Waziri wa Ujenzi Dokta JOHN MAGUFULI

Akijibu swali bungeni DODOMA, Dokta MAGUFULI amesema fedha hizo zitatolewa katika kipindi cha mwaka huu. 

Awali akijibu maswali ya wabunge Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa - TAMISEMI KASSIM MAJALIWA amesema miongoni mwa barabara zitakazojengwa katika utekelezaji wa ahadi za rais ni kwenye maeneo ya KILWA KIVINJE, Jimbo la MSALALA na NKENGE. 


Aidha Waziri MAJALIWA amesema fedha kwa ajili ya utekelezaji wa miradi mingine ya kijamii ambayo ni sehemu ya ahadi za rais pia zitatolewa kwa maeneo husika.


Sikiliza alichokisema Dokta John Magufuli...