Meneja wa Yanga SC, Hafidh
Saleh (kushoto) akimkabidhi jezi ya klabu hiyo, kiungo mpya Deus Kaseke (kulia)
leo makao makuu ya klabu, Jangwani, Dar es Salaam. Katikati ni Mkuu wa Idara ya
Habari na Mawasiliano ya klabu, Jerry Muro.
Kaseke amepewa jezi namba
nne iliyoachwa wazi na kiungo wa zamani wa timu hiyo, Athumani Iddi 'Chuji'
aliyeachwa misimu miwili iliyopita.
Kwasasa mlinzi kijana wa
Yanga, Rajab Zahir alikuwa anaitumia jezi hiyo, lakini wakati Kaseke
akitambulishwa rasmi leo na Yanga, makao makuu ya klabu hiyo, mitaa ya
Jangwani, Kariakoo, Dar es salaam, amepewa jezi hiyo.
Kwanini Deus Kaseke
amechagua jezi namba 4 kama ilivyokuwa Mbeya City?
Stori nyuma ya pazia ni
kwamba; Kaseke anampenda sana kiungo wa zamani wa Yanga, Athumani Idd ‘Chuji’
ambaye kwa muda mrefu amekuwa akitumia jezi namba 4.
Chuji ambaye alicheza
Yanga kwa mafanikio makubwa ni mchezaji kipenzi cha Kaseke, hivyo aliamua
kutumia jezi kama yake (namba 4) akiamini siku moja atafanikiwa kama nyota
huyo.
Mbali na kucheza Yanga,
Chuji pia alicheza Simba kwa mafanikio pamoja na timu ya Taifa ya Tanzania.
‘Kaka Mkubwa’ Chuji
kwasasa ni mchezaji wa Mwadui fc iliyopanda kucheza ligi kuu soka Tanzania
bara.