Monday, 25 May 2015

REAL MADRID YAMFUKUZA KAZI CARLO ANCELOTTI BAADA YA KUMALIZA MSIMU BILA YA TAJI


RASMI: Real Madrid imevunja mkataba na kocha wake Carlo Ancelotti baada ya kuinoa kwa miaka miwili.

Katika msimu wake wa kwanza Bernabeu, Ancelotti alishinda ligi ya mabingwa, Copa del Rey, Uefa Super Cup na kombe la klabu bingwa ya FIFA duniani.
Ancelotti ameshindwa kushinda medali msimu huu na kumaliza pointi mbili nyuma ya mabingwa FC Barcelona.

Kocha wa Napoli, Rafael Benitez anapewa nafasi kubwa ya kuchukua mikoba ya Ancelotti.

Rais wa Real Madrid, Florentino Perez amethibitisha kufukuzwa kwa Carlo na anatarajia kutangaza mrithi wake juma lijalo.