Bob junior ni msanii na
mproducer wa kwanza ambaye ndiye aliyerikodi album ya kwanza ya Diamond
Platnumz enzi hizo ikiongozwa na hits kama vile kamwambie na Mbagala lakini
baadae aligombana na kukaa miaka bila ya kuzungumza.
Lakini Diamond alitaka
amani na kutaka suluhu na Bob, japo ilifanikiwa wakakutana lakini mpango wa
Diamond haukufanikiwa… ishu ikaendelea mpaka juzi May 1 ambapo Bob junior alipotokea
kwenye Zari All White Part ndio maswali yakaanza kuulizwa, imekuwaje Bob ambaye
hapatani na Diamond kuhudhuria.
“Si mara ya kwanza kupata
mialiko kutoka kwa Diamond ila nikatafakari tulipotoka na wapi tunapokwenda na
ukiangalia tunafanya kazi moja so nikapata ushauri kutoka kwa makaka,mabibi,mababu
na watu wengi, wakaniambia nisahau yaliyopita na mimi nimesahau yote na kuanza
mapya” Alisema Bob alipohojiwa na Millard Ayo.com