Monday, 13 April 2015

MALI ZA GWAJIMA ZAANIKWA: Akisiwa Kuwa Mchungaji Tajiri Afrika!


Sakata la Gwajima limechukua sura mpya baada ya mchungaji huyo kutakiwa na jeshi la polisi kupeleka nyaraka mbalimbali zinazohusu umiliki wa mali zake!

Mchungaji Gwajima katika kupingana na amri hiyo halali ya jeshi la polisi, amekimbilia kwa mawakili, ili tu kuweka pingamizi la yeye kuthibitisha umiliki wake wa mali alizonazo na namna alivyozipata.


Itakumbukwa kuwa jeshi la polisi lilimtaka Gwajima apeleke nyaraka zifuatazo: Hati ya usajili wa kanisa lake, namba ya usajili wa kanisa lake, hati ya umiliki wa helikopta, hati za nyumba anazomiliki, idadi ya makanisa yaliyopo chini yake na taarifa za mapato na matumizi ya makanisa yake.


Nyaraka zingine ni: majina ya bodi ya udhamini wa kanisa na waraka wa maaskofu uliosomwa makanisani ambao Kardinali Pengo aliupinga!


Taarifa kuhusu mali za Gwajima ni hii hapa:


...Gwajima ana miliki nyumba nne za ghorofa Mbezi beach na kwa mujibu wa ripoti ya uthamini wa nyumba hizo jumla zina thamani ya bilioni 11 na milioni 400 (11.4 bilioni) pesa za Kitanzania.


...Pia ana nyumba nyingine kadhaa kwenye maeneo mbalimbali nchini ila hadi hivi sasa taarifa za uhakika za thamani ya nyumba hizo bado hazipo wazi.


...Gwajima ana miliki helikopta moja na magari ya kifahari kama vile Hammer, Range rover. Magari mengine ni Nissani Murano, Land Rover 4 na Land Cruiser V8.


...Gwajima pia amenunua magari mengine 40 yenye thamani kati ya Tshs 10 milioni na Tshs 20 milioni na kuwapatia wachungaji wake kote nchini kwa ajili ya shughuli zao binafsi na magari yote hayo yapo chini ya umiliki wake.


...Inakadiliwa kuwa akaunti binafsi za Gwajima zilizopo hapa nchini zina zaidi ya Tshs 20 bilioni ikiwa ni fedha zilizopo nje ya fedha za akaunti ya kanisa.


Aidha, pamoja na yeye mwenyewe kutaarifu juu ya mali zake kama ambavyo zimeorodheshwa hapo juu, lakini siku ya jana akiwa anahubiri kanisani kwake alikana kuwa yeye sio tajiri! 


Gwajima alikaririwa akisema kwamba mali zote anazomiliki ni baraka tu za Mungu na sio kwamba yeye ni tajiri. Gwajima alisisitiza kuwa yeye ni maskini kama walivyo maskini wengine wakiwemo wahumini wake, na wanaosema yeye ni tajiri wanawivu na wanamuonea. 


Source: HabariLeo