Mbunge wa Jimbo la Kigoma Kaskazini Zitto Kabwe leo March
14 ametoa gari mpya ya kubebea wagonjwa (Ambulance)kama moja ya ahadi zake
alipokuwa kwenye kampeni ambapo aliahidi kabla ya kumaliza kipindi cha uongozi
wake atatoa gari hiyo.
Wakipokea msaada huo Michael Mwandezi ambaye ni Mkurugenzi Mtendaji wa halmashauri ya Kigoma pamoja na Hamis Said Betese ambaye naye ni Mwenyekiti wa Halmashauri ya Wilaya ya Kigoma ambapo kwa niaba ya wananchi wa kata ya Nyarubanda ambao ndio msaada huo wamemshukuru sana Mbunge Zitto Kabwe..
Hata hivyo kabla ya kuelekea kukabidhi Gari hiyo ya kubebea wagonjwa,Zitto
Kabwe aliwatembelea Wanachama wa Chama cha Ushirika Rumaco ambao
wanajishughulisha na kilimo cha Kahawa kutoka kijiji cha Matyazo Kigoma
Kaskazini.
Zitto akiwa kwenye shamba lake la kahawa.