JESHI la Polisi Kanda Maalumu ya Dar es Salaam limeanza
kumchunguza Josephine Mushumbusi, ambaye ni mke wa Katibu Mkuu wa Chama cha
Demokrasia na Maendeleo (Chadema), Dk. Willibrod Slaa, anayetuhumiwa kula njama
za kumuangamiza.
Uchunguzi dhidi ya Mushumbusi ulitangazwa jana na Kamanda wa Polisi Kanda
Maalumu ya Dar es Salaam, Kamishna Suleiman Kova, katika mkutano wake na
waandishi wa habari uliofanyia ofisini kwake, Dar es Salaam.
Kamishna Kova alisema kuanzishwa kwa uchunguzi huo ni matokeo ya maelezo ya
Khalidi Kangezi, ambaye alikuwa mlinzi wa Dk. Slaa aliyefikishwa polisi baada
ya kuteswa na kutekwa kwa tuhuma za kushiriki mipango ya kumuua bosi wake huyo.
Alisema, Kangezi baada ya kufikishwa katika Kituo cha Polisi cha Oysterbay,
katika maelezo yake aliwataja Mushumbuzi na mchungaji mmoja ambaye jina lake
halijawekwa hadharani kuwa ndio waliokuwa na mpango huo, lakini yeye aliuzuia
Mbali na wawili hao, Kamanda Kova alisema uchunguzi huo pia utawagusa Makamu
Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), Philip Mangula, ambaye ametajwa na
baadhi ya makada wa chama hicho kuwa mmoja wa wahusika wa mpango wa mauaji ya
Dk. Slaa.
Wakati Jeshi la Polisi likitangaza kuanzishwa uchunguzi huo, wanachama
watatu wa Chadema wanaotuhumiwa kumteka na kumtesa Kangezi, jana walishtakiwa
katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu kwa kutenda makosa mawili.
Washtakiwa hao walisomewa mashtaka yao na Wakili wa Serikali, Janeth Kitali,
mbele ya Hakimu Mkazi Mkuu, Warialwande Lema, majira ya saa nane mchana.
Wakili Kitali alidai mahakamani hapo kuwa kosa la kwanza la washtakiwa, Diwani
Boniface Jacob (32), Mlinzi Hemedi Sabula (48) na Ofisa Utawala wa chama hicho,
Benson Mramba, ni kumjeruhi Kangezi, kosa ambalo walilitenda Machi 7, mwaka
huu.
Katika shtaka hilo washtakiwa wanadaiwa kwamba tarehe hiyo wakiwa Makao Makuu
ya Ofisi za Chadema zilizopo Mtaa wa Ufipa, Kinondoni Dar es Salaam,
walimjeruhi Kangezi kwa kumshambulia sehemu mbalimbali za mwili wake na
kumsababishia maumivu makali.
Aliendelea kudai kuwa tarehe na eneo walipofanya kosa la kwanza, walitenda kosa
jingine la kumteka Kagenzi na kumpeleka katika Hotel ya River View Hotel
iliyopo Sinza, Kinondoni, Dar es Salaam, kwa nia ya kumnyima uhuru wake
Washtakiwa hao wanaotetewa na Wakili Peter Kibatala na John Malya, walikana
mashtaka yote na upande wa mashtaka ulidai kuwa upelelezi wa kesi hiyo
haujakamilika, hivyo kesi iliahirishwa hadi Machi 26 mwaka huu, itakapotajwa
tena.
Hakimu Lema aliwataka washtakiwa kuwa na wadhamini wawili kila mmoja ambao
wanatoka katika taasisi inayotambulika au serikalini isipokuwa walimu.
Wadhamini hao walipaswa kusaini hati ya dhamana ya maandishi ya Sh milioni 10.
Washtakiwa walishindwa kutimiza masharti ya dhamana na kupelekwa gereza la Keko
hadi hapo upande wa mashtaka utakapomaliza kufanya ukaguzi wa barua za
wadhamini wao kuona kama wamekidhi vigezo.
Kabla ya kupandishwa kizimbani kwa washtakiwa hao, Kamishna Kova aliwaambia
waandishi wa habari kuwa kitendo cha makada watano wa Chadema cha kumuweka
chini ya ulinzi na kumtesa kwa muda wa saa 15 Kangezi ni kosa kisheria, hivyo
Jeshi la Polisi limewafunguliwa shauri la kushambulia hadi kumjeruhi mlinzi
huyo.
Kova alisema Jeshi la Polisi limechukua uamuzi huo kutokana na maelezo pamoja
na majeraha aliyoyapata Kangezi mara baada ya kufikishwa katika Kituo cha
Polisi cha Oysterbay.
Alisema, ingawa Wakili wa Chadema, John Malya alimfikisha Kangezi katika Kituo
cha Polisi cha Oysterbay na kumfungulia shitaka la kupanga njama za
kumuangamiza Dk. Slaa kwa kumuwekea sumu kwenye maji au chakula, Kangezi kwa
upande wake alitoa maelezo ya kutekwa nyara na makada watano wa Chadema ambao
walimuweka chini ya ulinzi na kumtesa hadi kumuumiza.
“Tumefungua mashauri mawili, la kwanza ni uchunguzi dhidi ya tuhuma na mpango
wa kutaka kumdhuru Dk. Slaa na pili ni uchunguzi dhidi ya watuhumiwa wanaodaiwa
kumtesa kwa kumshambulia Kangezi na kumsababishia majeraha mwilini mwake,”
alisema Kamishna Kova.
Kamishna Kova alisema kutokana na maelezo ya Kangezi, Jeshi la Polisi
linaendelea kuwasaka watuhumiwa waliotajwa na Kangezi kuhusika kumtesa na
kumteka.
Alisema baada ya uchunguzi wa awali wa mashauri yote mawili kukamilika,
yatapelekwa kwa Wakili wa Serikali ili wote wanaohusika katika suala hilo
wafikishwe mbele ya sheria.
Chanzo:Mtanzania
Uchunguzi dhidi ya Mushumbusi ulitangazwa jana na Kamanda wa Polisi Kanda Maalumu ya Dar es Salaam, Kamishna Suleiman Kova, katika mkutano wake na waandishi wa habari uliofanyia ofisini kwake, Dar es Salaam.
Kamishna Kova alisema kuanzishwa kwa uchunguzi huo ni matokeo ya maelezo ya Khalidi Kangezi, ambaye alikuwa mlinzi wa Dk. Slaa aliyefikishwa polisi baada ya kuteswa na kutekwa kwa tuhuma za kushiriki mipango ya kumuua bosi wake huyo.
Alisema, Kangezi baada ya kufikishwa katika Kituo cha Polisi cha Oysterbay, katika maelezo yake aliwataja Mushumbuzi na mchungaji mmoja ambaye jina lake halijawekwa hadharani kuwa ndio waliokuwa na mpango huo, lakini yeye aliuzuia
Mbali na wawili hao, Kamanda Kova alisema uchunguzi huo pia utawagusa Makamu Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), Philip Mangula, ambaye ametajwa na baadhi ya makada wa chama hicho kuwa mmoja wa wahusika wa mpango wa mauaji ya Dk. Slaa.
Wakati Jeshi la Polisi likitangaza kuanzishwa uchunguzi huo, wanachama
watatu wa Chadema wanaotuhumiwa kumteka na kumtesa Kangezi, jana walishtakiwa katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu kwa kutenda makosa mawili.
Washtakiwa hao walisomewa mashtaka yao na Wakili wa Serikali, Janeth Kitali, mbele ya Hakimu Mkazi Mkuu, Warialwande Lema, majira ya saa nane mchana.
Wakili Kitali alidai mahakamani hapo kuwa kosa la kwanza la washtakiwa, Diwani Boniface Jacob (32), Mlinzi Hemedi Sabula (48) na Ofisa Utawala wa chama hicho, Benson Mramba, ni kumjeruhi Kangezi, kosa ambalo walilitenda Machi 7, mwaka huu.
Katika shtaka hilo washtakiwa wanadaiwa kwamba tarehe hiyo wakiwa Makao Makuu ya Ofisi za Chadema zilizopo Mtaa wa Ufipa, Kinondoni Dar es Salaam, walimjeruhi Kangezi kwa kumshambulia sehemu mbalimbali za mwili wake na kumsababishia maumivu makali.
Aliendelea kudai kuwa tarehe na eneo walipofanya kosa la kwanza, walitenda kosa jingine la kumteka Kagenzi na kumpeleka katika Hotel ya River View Hotel iliyopo Sinza, Kinondoni, Dar es Salaam, kwa nia ya kumnyima uhuru wake
Washtakiwa hao wanaotetewa na Wakili Peter Kibatala na John Malya, walikana mashtaka yote na upande wa mashtaka ulidai kuwa upelelezi wa kesi hiyo haujakamilika, hivyo kesi iliahirishwa hadi Machi 26 mwaka huu, itakapotajwa tena.
Hakimu Lema aliwataka washtakiwa kuwa na wadhamini wawili kila mmoja ambao wanatoka katika taasisi inayotambulika au serikalini isipokuwa walimu. Wadhamini hao walipaswa kusaini hati ya dhamana ya maandishi ya Sh milioni 10.
Washtakiwa walishindwa kutimiza masharti ya dhamana na kupelekwa gereza la Keko hadi hapo upande wa mashtaka utakapomaliza kufanya ukaguzi wa barua za wadhamini wao kuona kama wamekidhi vigezo.
Kabla ya kupandishwa kizimbani kwa washtakiwa hao, Kamishna Kova aliwaambia waandishi wa habari kuwa kitendo cha makada watano wa Chadema cha kumuweka chini ya ulinzi na kumtesa kwa muda wa saa 15 Kangezi ni kosa kisheria, hivyo Jeshi la Polisi limewafunguliwa shauri la kushambulia hadi kumjeruhi mlinzi huyo.
Kova alisema Jeshi la Polisi limechukua uamuzi huo kutokana na maelezo pamoja na majeraha aliyoyapata Kangezi mara baada ya kufikishwa katika Kituo cha Polisi cha Oysterbay.
Alisema, ingawa Wakili wa Chadema, John Malya alimfikisha Kangezi katika Kituo cha Polisi cha Oysterbay na kumfungulia shitaka la kupanga njama za kumuangamiza Dk. Slaa kwa kumuwekea sumu kwenye maji au chakula, Kangezi kwa upande wake alitoa maelezo ya kutekwa nyara na makada watano wa Chadema ambao walimuweka chini ya ulinzi na kumtesa hadi kumuumiza.
“Tumefungua mashauri mawili, la kwanza ni uchunguzi dhidi ya tuhuma na mpango wa kutaka kumdhuru Dk. Slaa na pili ni uchunguzi dhidi ya watuhumiwa wanaodaiwa kumtesa kwa kumshambulia Kangezi na kumsababishia majeraha mwilini mwake,” alisema Kamishna Kova.
Kamishna Kova alisema kutokana na maelezo ya Kangezi, Jeshi la Polisi linaendelea kuwasaka watuhumiwa waliotajwa na Kangezi kuhusika kumtesa na kumteka.
Alisema baada ya uchunguzi wa awali wa mashauri yote mawili kukamilika, yatapelekwa kwa Wakili wa Serikali ili wote wanaohusika katika suala hilo wafikishwe mbele ya sheria.
Chanzo:Mtanzania