Saturday, 9 May 2015

Tetesi: Jokate na Alikiba Wadaiwa Kuzama Penzini

Tetesi  za mastaa wa hapa Bongo, Jokate Mwegelo na Ally Kiba kuwa kwenye mahusiano ya kimapenzi zimezidi kupamba moto baada ya hapo jana mtangazaji wa Clouds FM Soudy Brown kumuoji Jokate juu ya ukweli wa tetesi hizo ambapo Jokate aliishia kucheka tu bila kutoa majibu.

Kwa mujibu wa Soudy kwa muda mrefu amekuwa akiwafuatilia wa wili hao kwani mara nyingi wamekuwa wakionana  wakiwa pamoja sehemu mbalimbali  kama kwenye restaurants na mara kadhaa nyumbani kwa Alikiba.

Sasa leo kwenye mitandao ya kijamii, kumekuwa na picha hiyo hapo juu ikimuonyesha Jokate  akiwa metinga kofia ya mkeke ya Ally Kiba
Bado  lakini wadaku waneendelea kuunganisha ‘DOTS’ ukweli utafahamika tu.
Mzee wa Ubuyu

Kuna tetesi zinavuna kuwa Jokate Mwegelo na Alikiba ni wapenzi!