Mwili wa mwanamke ni tofauti na wa mwanaume linapokuja swala la kujamiiana. Mwanaume ni rahisi sana kupata ashki hasa akiona mwili wa mwanamke ukiwa uchi. Mwanaume anachohitaji ili apate ashki ni kuwaza ngono, pamoja na kuona mwili wa mwanamke, hiyo inatosha kumuweka tayari kwa tendo la kujamiiana. Kwa kawaida mwanaume huwa anapata ashki kwenye maeneo yake ya siri peke yake na siyo mwili mzima kama ilivyo kwa mwanamke.
Mwanamke yeye ili aweze kupata ashki na awe tayari kufanya tendo, inatakiwa aandaliwe vya kutosha, kwani mwili wake wote unatakiwa upate ashki na siyo sehemu zake za siri peke yake kama ilivyo kwa mwanaume. Kuamsha sehemu za siri za mwanaume ni rahisi sana, ni eneo dogo, na huchukua muda mfupi sana, chini ya dakika moja.
Lakini kuamsha mwili wa mwanamke ili uwe tayari kufanya ngono siyo rahisi kufanya hicho, inahitaji muda mrefu, zaidi ya dakika tano mpaka saa moja au zaidi kutegemea aina ya maandalizi au aina ya mwanamke. Kwa hiyo wanaume wanatakiwa wafahamu tofauti hizi, ili kupunguza lawama zipungue kama sio kuzifuta kabisa, na mimi ninaamini ipo siku zitaisha kwa kadiri dunia hii inavyozidi kuwa ndogo mfano wa kijiji.
Kwa kawaida baadhi ya wanaume huwa na haraka sana, huwa wana
papara sana, na sijui huwa wanataka kuwahi nini na wapi. Mwanaume huwa hana
subira wakati wa kufanya ngono, anataka afanye haraka, amalize kisha ageukie
ukutani. Sijui huko ukutani huwa kuna nini, huu ni ukatili, haukubaliki.
Haitakiwi mwanaume amwingilie mwanamke kama mwanamke hajawa tayari kwa tendo.
Maandalizi kabla ya ngono ni jambo muhimu sana kuliko hata ngono yenyewe. Kama
maandalizi yakiwa mazuri utaifurahiya ngono, lakini maandalizi yakiwa hafifu
huwezi kuifurahia ngono.Kuna njia nyingi sana za kumuandaa mwanamke, nitazitaja
chache.
Mojawapo ni njia ya mazungumzo, mwanaume anatajkiw aaongee na mpenzi
wake kwa lugha nzuri, kwa maneno matamu na yenye mahaba. Atumie muda mwingi kuzungumza
naye, asiwe na haraka kuanza kufanya ngono.
Mazungumzo yahusu masuala ya
uhusiano ukiwemo upenzo. Usizungumzie madeni yako unayodaiwam, usizungumzie
matatizo yako au ya familia yenu. Baadhi ya wanwake wanaweza kujisikia
kujamiiana kutokana na mazungumzo peke yake. Lakini pia kuna baadhi ya wanwake
wengine ambao huwa hawapendi kufanya ngono unapokutana nao kwa mara ya kwanza,
wanataka tu mzungumze tu na si zaidi ya hapo.
Jambo hili kwa wanaume walio wengi
ni gumu sana, wao wantaka ngono siku hiyo hiyo ya kwanza. Sisemi kufanya hivyio
ni vibaya au vizuri, inategemea mazingira na makubaliano yenu.
Njia ya pili ni ya kumshikashika sehemu mbalimbali za mwili wake. Njia
hii inaweza kwenda sambamba na ile ya kwanza. Wakati unamshikashika usitumie
nguvu, mshike kama vile unampapasa.
Achana na mambo yote uliyoambiwa na
rafiki zako kwamba mwanamke ukimshika sehemu Fulani ndio anajisikia kufanya
ngono, huu ni utoto, ni ukasuku.
Wanwake wote wanatofautiana.
Linapokuja swala la kujamiiana mwili wa mwanamke unaweza kuufananisha na dunia
hii tunayoishi. Una milima na mabonde, mito, maziwa na bahari, una mbuga za
wanyama kwa kifupi ni kwamba, una kila kitu unachokiona hapa duniani, ni juu ya
mwanaume kuwa mvumbuzi wa maeneo mbalimbali atakayoyatumia kumuandaa mwanamke
aliye naye ile awe tayari kufanya ngono na kufika kileleni kwa urahisi.
Wakati mwanaume anaendelea na
utafiti huo wa kumuandaa mwanamke anatakiwa awe macho na atumie milango yake
sita ya fahamu.(Najua kuna wazo limekuambia nimekose) Sijakosea, milango ya
fahamu ipo sita na siyo mitano kama ulivyofundishwa. Mwanaume anatakiwa atumie
milango yote sita ya fahamu ili kujua ni maeneo gani anapoyagusa yanamfanya
mwanamke ajisikie vizuri zaidi, yanamfanya asisismke. Pia ni maeneo gani
akiyagusa yanamfanya ajisikie vibaya.
Mwanaume anatakiwa apelike
uzingativu wake kwenye yale maeneo yanayomfanya mwanamke ajisikie vizuri. Kwa
kawaida, maeneo Fulani yanaweza yakamfanya mwanamke Fulani ajisikie vizuri,
lakini maeneo hayo hayo ukimshika mwanamke mwingine anajisikia vibaya au
anakereka. Haitakiwi mwanaume akariri maeneo yanayoleta msisimko mmoja na
kuyatumia kw amwanamke mwingine, hiyo si sawa. Kwa hiyo mwanaume anatakiwa
aachane na mazoea, wakati wa kumuandaa mwanamke na badala yake anatakiwa awe
mvumbuzi kama Dr. Livingstone.
Kila siku mwanaume anatakiwa
ahakikishe anavumbua maeneo mapya, milima mipya, mito mipya, mbuga mpya,
bustani mpya, bahari mpya, …nk. Nilisema mwili wa mwanake ni kama dunia, hivyo
mwanume hatakiwi atosheke na maeneo aliyoyagundua, kila siku anatakiwa agundue
maeneo mapya yanayoleta msisimko kwa mwenzi wake. Je utajuaje kwamba sasa
mwanamke yupo tayari kwa tendo…..?
Baadhi ya dalili utakazoziona ni
mabadiliko katika upumuaji, sehemu zake za siri, matiti, kkijasho chembamba
kwenye ngozi. Lakini kwa kuwa wewe ni mvumbuzi, hakikisha unavumbua nyingine
nyingi zaidi. Ukweli ni kwamba zipo nyingi mno, usikariri, kila mwanamke ana
dalili zake, kuna uwezekano mkubwa zikatofautiana. Baada ya kuona dalili hizo,
ndipo tendo linaweza kufanyika….. Kufika kileleni……..!
Jambo la kwanza litakalokuwezesha
kufika kileleni ni kufuta kwenye akili yako yale mambo yote hasi uliyoambiwa na
jamii kwamba ngono ni mbaya, ngono ni dhambi, ngono ni uchafu. Anza kuiona
ngono ni tendo takatifu, ni kitu kitakatifu, ni tendo la uumbaji, ni zawadi
kutoka kwa Mungu. Jambo la pili ni kutoruhusu akili yako kuingilia wakati
unafanya ngono.
Kama kitanda kinapiga kelele, kiache
kipige kelele, kama unajisikia kulia wakati unafanya ngono usijizuie, bali lia.
Ukijisikia kupiga makelele, piga, usijizuie. Kama utajisikia kunyanyua miguu
juu au mikono, usijizuie, we nyanyua tu.
- Uache mwili ufanye chochote unachotaka kufanya. Usiiruhusu akili yako kuingilia kwa namna yoyote wakati unafanya ngono.
- Usiwe mshiriki na badala yake unatakiwa uwe mtazamaji. Unatakiwa uwe mshuhudiaji wa mwili wako na tendo lote kwa ujumla.
- Uwe kama mtu anayetazama mpira uwanjani na siyo mchezaji.
Wakati unaendelea na ngono usiiruhusu
akili yako ikaanza kuwaza kwamba, huyu mpenzi uliye naye ni mzuri au mbaya,
anajua mapenzi au hajui, leo nitafaidi au sitafaidi, sijui nitamridhisha, sijui
nitaambukizwa ukimwi au magonjwa ya zinaa, sijui nitapata mimba, sijui kondom
itapasuka, sijui kuna watu wanatuchungulia huko nje, sijui haya maumbile yake
makubwa yataniumiza….. yaani akili yako inatakiwa ijiepushe na mawazo ya aina
hiyo au yanayofanana na hayo. Kama akili yako imejaa mawazo ya aina hiyo, ni
vigumu sana kufika kileleni. Ukweli ni kwamba huwezi kufurahia ngono hata
kidogo, sana sana utatoa manii tu basi…
Hizi ni dondoo nilizotoa katika
kitabu kipya kiitwacho “Zijue siri zilizojificha ndani ya tendo la
kujamiiana.”Kitabu hicho kimeandikwa na mwanautambuzi Dr. Simbila Nkelege,
akishirikiana na wana FAJI. Kama unakihitaji kitabu hiki ni PM, kitakufuata
hapo ulipo
Source: DarasaHuru