Monday, 16 March 2015

FAIZA ALLY Awajibu Wambea Kuhusu SUGU na Mwanaye na Kuhusu Ndoa yao Kuvunjika



Sugu na mwanawe
 
MSANII wa filamu Faiza Ally ambaye amezaa na Mbunge wa Mbeya mjini, Joseph Mbilinyi ‘Sugu’, leo amewatolea uvuvi watu waliokuwa wakijiuliza maswali kuhusu mwanaye Sasha na na baba yake.

Kupita akaunti yake ya Instagram, Faiza ameweka picha na Mhe. Sugu akiwa na mwanaye Sasha na kuandika kuwa    

"Mara nyingi huwa nawapiga picha mimi mwenyewe sema tu sipendi sana kurusha kwangu"

Na kwa wale waliokuwa wanauliza maswali juu yao, Faiza amewajibu hivi: "Ni kweli kuna wakati tulikuwa hatuelewani kabisa na wala hatukuwa tunaonana lakini kwa sasa tofauti zetu zimeisha hatuna ugomvi japo hatuko pamoja"
 


"Lakini mwisho wa siku huyo ndiyo baba Sasha na mzazi siku zote atakuwa mzazi tu, haijalishi tuna tofauti kiasi gani" Alimalizia kuandika msanii huyo asiyeishiwa vituko.

Baada ya kuwek picha hiyo wengi wa mashabiki wa Faiza walimpongeza kwa hatua hiyo huku wengine wakiwataka warudiane ili walee mtoto pamoja.