Tuesday 10 March 2015

AMINI: SIOGOPI KUIBIWA MKE

 Msanii wa Bongo Fleva, Amini Mwinyimkuu akiwa na mkewe.

BAADA ya mke wa msanii wa Bongo Fleva, Amini Mwinyimkuu, Farida kujitosa kwenye muziki huo, mumewe ameibuka na kusema kuwa kamwe haogopi kuibiwa na wakware.Akipiga stori na Over The Weekend, Amini alisema mke wake ni muimbaji mzuri sana na ndiyo sababu iliyomfanya amshirikishe kwenye wimbo wake mpya anaotarajia kuuachia hivi

karibuni.“Nikiweka fikra za kuibiwa mke hatutasonga kimuziki wala kimaisha na kwa sababu hakuna kitakachokuwa kikiendelea kati yetu, mimi namuamini na yeye ananiamini vilevile na mambo kama hayo hayatakuwa na nafasi kwetu kama tukishikamana vizuri,” alisema Amini.

Mbali na hayo Amini aliendelea kufunguka kuwa kama kuna msanii atahitaji kufanya kolabo na mkewe basi inabidi amsikilize kwanza na kisha waelewane juu ya hilo bila kusahau kumtangaza kimuziki.