Kundi
la muziki wa bongo flava nchini, Yamoto Band wanatarajia kukwea pipa kwenda
Afrika Kusini kwa ajili yakufanya video ya wimbo wao ‘Cheza kwa Madoido’ na
muongozaji mahili barani Afrika, Godfather.
Yamoto Band ambao usiku wa kuamkia jana walitwaa tuzo ya Kili katika kipengele
cha ‘Kikundi bora cha muziki (Bongo Flava) wameamua kwenda Afrika Kusini
kufanya video ikiwa ni hatua za awali za kuingia katika soko la kimataifa.
Aidha Yamoto Band wameachia video ya wimbo wao mpya unaoitwa ‘Nisambazie Raha’
unaofanya vizuri sana katika vituo vya radio iliyofanyika chini ya uongozaji
wake Isangi Mental.