Moja kati ya show za
muziki wa Bongo Flava zilizokuwa zinatolewa na kituo cha EA radio ni Planet
Bonggo kikiwa kinaendeshwa na Abdallah Wambua aka Dullah, kwa habari hii ni
pigo sana kwenye tasnia ya muziki wa Bongo Flava kwasababu Planet Bongo
inayorukua kila siku ya jumamosi ililete mwanga mkubwa na kuinua muziki wa
kizazi kipya kwa kuupa airtime ya kutosha.
Taarifa hiyo imekuja baada
ya kusambaa kwenye mitandao ya kiamii kuwa mwisho wa kipindi cha Planet Bongo
ni jumamosi ya kesho, hapa Dullah akifunguka zaidi
“Ni miaka saba (7) sasa tangu nianze kutangaza kwenye kipindi cha Planet Bongo tangu mwaka 2008, tumefanya mengi mazuri katika kuutetea huu muziki wa kizazi kipya. Hii ni ngumu sana kusema hichi ninacotaka kukwambia ila ndo hali halisi.. Jumamosi hii ndio mwisho wa Planet Bongo ya EA radio.
Nitawamiss sana wote tuliokuwa tukisikilizana kila jumamosi, TUKUTANA JUMAMOSI HII KATIKA KUAGANA RASMI #PlanetBongoIsDead.
Alikipost salama Jabir Katika akaunt yake ya twitter hiki hapa;