Baada ya kufungwa mfululizo kwa timu ya Taifa, Taifa Stars
hatimaye kocha mkuu wa timu hiyo Maart Nooij ametimuliwa kazi ya kuendelea kukinoa kikosi hicho.
Kamati ya utendaji ya Shirikisho la soka Tanzania TFF katika kikao chake
kilichokaa jana usiku kimefikia uamuzi huo wa kumsimamisha kazi kocha huyo
kuanzaia leo June 21 pamoja na kuvunja benchi la ufundi la timu hiyo.
TFF imeahidi kutangaza wakati wowote benchi jipya la
ufundi la timu hiyo.
Stars iliambulia kipigo cha mabao 3-0 dhidi ya Uganda jana
katika uwanja wa Amaan ikiwa ni mechi ya kwanza ya kufuzu mashindano ya CHAN
2016 yatakayofanyika Rwanda.