Mtangazaji wa Kipindi cha
Take One, kinachorushwa kupitia Clouds TV, Zamaradi Mketema ‘Zama’ amefunguka
kuwa, ataongeza tena watoto kwani tangu amejifungua mtoto wa pili ameona nyumba
imekuwa na raha sana.
Akipiga stori na Ijumaa hivi karibuni, Zamaradi alisema, ameshangazwa na furaha iliyotawala kwake na mzazi mwenzake na kwamba siku si nyingi atabeba mimba nyingine mbili fasta.
“Yaani watoto ni furaha
kubwa, mimi nitaongeza tena wawili wa haraharaka maana nimegundua kuna kitu
kinaongezeka kila unapoongeza mtoto mwingine ndani ya nyumba ikiwa ni pamoja na
baraka,” alisema Zamaradi.