BABA mzazi wa Meneja wa Nasibu Abdul ‘Diamond’, Babu Tale, amezikwa
juzi Jumanne kijijini kwao Mkuyuni, mjini Morogoro lakini miongoni mwa mambo ya
kushangaza ni kitendo cha baadhi ya waombolezaji kumsaka mwanamuziki Nasibu
bila mafanikio.
Hilo lilijitokeza baada ya msafara uliotokea Dar kufika eneo hilo ambapo vijana walilizingira gari lililokuwa na mastaa na kuanza kuuliza juu ya uwepo wa Diamond.Vijana hao waliotarajia kumuona msanii huyo msibani hapo, hata waliposikia tetesi kuwa hakuwepo, waliendelea kumsaka kila gari huku wakimuuliza kila waliyemuona lakini jibu lilikuwa lilelile, hakufika.
Majibu hayo yalionekana kuwanyong’onyesha vijana hao ambapo
baadhi waliamua kuondoka kuonesha dhahiri kuwa kilichowapeleka pale ni kumuona
Diamond na si kuzika.Hata hivyo, vijana wengine waliamua kujipoza kwa kupiga
picha na Madee kisha kushiriki mazishi hayo mwanzo mwisho.