Mjengo anaoishi mkali wa
Bongo Fleva anayetamba na ngoma yake ya Chekecha Cheketua, Ali Saleh Kiba
uliopo Kunduchi-Mbezi Beach jijini Dar, unadaiwa kuzua utata mkubwa hivyo
kulilazimu Risasi Jumamosi kuchimba na kubaini kuwa nyumba hiyo si ya msanii
huyo bali amepangisha.
Nyumba anayoishi Alikiba kwa sasa.
Ilidaiwa kwamba, mara tu baada ya Kiba kutangaza kumiliki nyumba hiyo, ilidaiwa kuwa aliibuka mwanamke aliyetajwa kwa jina moja la Mariana ikisemekana eti ndiye mmiliki halali wa nyumba hiyo.Madai mazito yaliendelea kushushwa kwamba, Mariana, akiwa mwandani wa Kiba ndiye aliyemuweka Kiba aishi kwenye nyumba hiyo wakati yeye (Mariana) kwa sasa anaishi nchini Singapore barani Asia.
“Ninyi mnasema ule mjengo ni wa Ali (Kiba)? Acheni hizo, kwa taarifa yenu hiyo nyumba kapewa na mrembo f’lani hivi amazing, anaitwa Mariana, ni Mbongo anayeishi Singapore.
“Muulizeni huyo Kiba awaambie ukweli,” kilisema chanzo chetu kikisisitiza: “Hata Mariana aliposikia eti nyumba ni ya Ali (Kiba) alishangaa na akamaindi ile mbaya hivyo kwa sasa sidhani kama wanaelewana kwa ajili hiyo.”
Baada ya kukutana na mkanganyiko huo, gazeti hili lilimtafuta Kiba ambaye alikiri kwamba kweli nyumba hiyo siyo yake bali amepangisha huku akikana kusema kuwa anaimiliki.Alipoulizwa juu ya madai ya kupewa nyumba hiyo na mwanamke aitwaye Mariana, Kiba alisema hayo ni maneno tu kwani anachojua yeye amepangisha.
“Kwanza hebu nitumie picha nijue ni nyumba gani?” aliomba Kiba ambapo alitumiwa picha kwa WhatsApp ndipo akajibu:
“Okey, kama ni hiyo nimepangisha lakini siyo kwamba sina nyumba.”
Source:GPL